Tuesday, March 4, 2014

HILI TANGAZO LINAWAHUSU WALE WANAOTAKA KURUDIA MTIHANI NA KUSOMA QT
BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA

 

TANGAZO

Kaimu Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwatangazia watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT)  mwezi Novemba,  2014  kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba kipindi cha usajili kwa malipo ya  ada ya kawaida (Shilingi 50,000/=kwa wanaojisajili CSEE na Shilingi 30,000/= kwa wanaojisajili QT ) kimeongezwa kutoka tarehe 28 Februari, 2014 hadi tarehe   31 Machi, 2014. Watahiniwa watakaojisajili  kuanzia tarehe 1 Aprili, 2014 hadi tarehe 30 Aprili, 2014 watatakiwa kulipa ada ya kawaida pamoja na faini mpaka usajili utakapofungwa rasmi tarehe 30 Aprili, 2014.

Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya Baraza la Mitihani ya www.necta.go.tz. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (reference number) zinazotolewa bure na kulipa ada ya mtihani kwa njia ya Posta au Mpesa.

 

Imetolewa na:

KAIMU KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA.

No comments:

Post a Comment