Monday, February 3, 2014

SHILOLE AKIRI LIVE REDIONI KUWA ANAYACHUNA MABUZI KAMA KAWA KAMA DAWA....!

 MSANII wa muziki wa Kizazi Kipya na Filamu Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’,jana alianika wazi tabia yake ya uchunaji mabuzi alipokuwa kwenye moja ya mahojiano na watangazaji wa Kipindi cha Leo tena cha Clouds FM, baada ya kuulizwa swali liloendana na jina la kibao chake kipya ambacho jana ndiyo ilikuwa siku rasmi akikiachia hewna kupitia stesheni za radio hiyo,baada ya kuachia ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la NACHUNA BUZI...
 
Mmoja ya watangazaji wa kipindi hicho alimuuliza ni kitugani kilichompelekea hadi kutunga wimbo wa namna hiyo na kuupa jina hilo,Shilole katika majibu yake alisema kuwa ameamua kukipa jina hilo kufuatia historia mbalimbali za maisha yake,hususani wimbo wake uliopita ambao aliupa jina la Nakomaa na jiji la Dar,sasa kudhihirisha kauli hiyo ameamua kuchuna mabuzi ili aweze kupata mkwanja wakutosha kulihimili jiji la Dar es Salaam na Igunga abaki kwenda kusalimia ndugu na jamaa tu. Baada ya maneno hayo Shilole pia aliandika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram:- 
shilolekiunoASANTENI MASHABIKI WANGU WOTE KWA KUIPOKEA VEMA NYIMBO YANGU MPYA#CHUNABUZI# MUNGU AWABARIK# AMEEN

No comments:

Post a Comment