Sunday, February 2, 2014

HIKI NDICHO KINACHOIUWA ORIJINO KOMEDY YA TBC

 

origino_komediMiaka mitatu au minne iliyopita ukimuuliza mtu ni show gani hauwezi kuikosa basi utasikia “ebwanae , mi siku ya alhamisi hata kama nina kazi siwezi kukosa show ya ze comedy”. kadiri siku zinavyoenda ndio mambo yanazidi kwenda mramba kwa kundi hili la vichekesho na hizi ndio sababu ambazo tunaweza kusema zinaliua kundi hili…

Kukosa Creativity

Siku hizi kuna some episodes unaweza kuangalia mwanzo mwisho na usicheke , kikubwa kinachosababisha hali hii ni creativity yaani ubunifu katika kuandika show yenyewe. kwa mfano segemnt kama laprofesoli ilibidi iwe ni ya wiki moja sababu wiki inayofata watazamaji wanakua wameshajua ni nini kitafanyika.

Orijino-Komedi

Kushiba pesa

Waigizaji wa orijino komedi wa sasa sio kama wale wa zamani ambao walikua wanategemea mshahara ili waweze kuendesha maisha yao. kwasasa kila mtu ana biashara yake ,na mishemishe nyingine kitu kinachowafanya wasiweke akili zao zote katika kuwafanya watu wavunje mbavu.

komedi-pesa

Matangazo ndani ya show

Kitendo cha kupata wadhamini na kuwalazimisha watangaze biashara yao ndani ya show kinachangia sana kuiua hii show. kwasasa unakuta asilimia 40 ya show ni matangazo, kama hawajatangaza mbuga za wanyama basi wameigiza tangazo la salama kondom.

matangao

Kutokuenda na matukio

zamani utakuta kama tukio kubwa limetokea wiki hii basi hautakosa kipindi cha ze comedy sababu unajua lazima uvunje mbavu kwa jinsi jamaa watakavyohusisha na tukio halisi.

comedy-rais-kikwete

Darasa na sio vichekesho tena

Hapa naongelea segments zao za siku hizi ambazo zinabadilisha maana ya kua shoo ya vichekesho na kuifanya iwe ni kama kipindi fulani cha kutoa elimu kwa mfano mbuga za wanyama na makavu laivu.

makavu laivu

Kubebwa na majina

sio siri kwasasa waigizaji wa ze komedi ndio waigizaji wa michezo ya televisheni wanaoongoza kwa kuwa na majina makubwa katika tasnia hii. Majina pia yamewafanya wabweteke nakuamini hata kama wasipochekesha shoo nzima watu lazima wawaangalie .

komedi

Kugundulika kwa vipaji vingine

Ukiachana na kazi ndani ya orijino komedi wengine wamegundua wanaweza kufanya vitu zaidi , wasanii zaidi ya mmoja ni wanamuziki sasa na tayari wana video zao na wengine hata album.

masanja album

Kukosekana kwa ushindani

wakati eatv wanafanya audition za kipindi kipya cha vichekesho baada ya ze comedy kuamia TBC watu wengi walitegemea ushindani katika tasnia hii lakini mambo yaawa ndivyo sivyo . Kama likitokea kundi jingine linaloweza kumalizia huu msiba ambao wengi wameshauona ukija basi ndio itatulazimu kulizika kundi hili na ikawa historia.

Cha msingi ni kwamba kuna uwezekano wa kubadilika , so inabidi jamaa wajipange upya na kama wakifanyia kazi mambo tuliyoyaongelea basi tutaanza kutoroka ofisini tuwahi saa 1 kuangalia orijino komedi.

No comments:

Post a Comment