Sunday, February 9, 2014

ALICHOKISEMA JOH MAKINI NA NIKKI WA II JUU YA VIDEO YAO ‘NJE YA BOX’ KUCHEZWA CHANNEL O.

Jana ilikuwa siku nzuri kwenye historia ya muziki ya kundi la Weusi linaloundwa na wasanii watano kutoka Kaskazini mwa Tanzania, Arusha, baada ya video ya wimbo wao ‘Nje ya Box’ kuchezwa Channel O.
Joh Makini aka Mwamba wa Kaskazini anaamini walichelewa tu kufika hapo walipofika, lakini pia akawashukuru wale wote waliofanikisha wao kufika pale walipofika.
Ameeleza pia sababu zilizomfanya achelewe kufika hapo na kudai kuwa kutokuwepo umoja kati ya wasanii wa Tanzania kuzisukuma kazi zao ni moja ya kikwazo, na kuutolea mfano umoja uliopo kati ya wasanii wa Nigeria ambao umewawezesha kuiteka Afrika na kuvuka mipaka.
“Sipendi sana kulaumu watu, lakini…unajua wenzetu Nigeria wanatupiga bao kwa sababu wenyewe nchi nzima wanafanya kazi kama timu moja.” Joh Makini ameieleza tovuti ya Times Fm.
Rapper huyo ameeleza pia kuhusu jinsi walivyojipanga kuendelea kumaintain level waliyofikia na mpango wa video ya wimbo wa Gere.
“Sisi Weusi ni watu ambao tunavunja rekodi zetu, ni lazima uweze kuvunja rekodi zako mwenyewe ili uweze kuendelea mbele. Kwa hiyo kazi yeyote nyingine itakayokuja baada ya Gere itavunja rekodi ya Gere. Unajua Nje ya Box imetimiza kile ambacho tuliiagiza kufanya. Kwa hiyo hatuwezi kubaki kwenye Nje ya Box siku zote.

“Nyuma ya Nje ya Box kuna Bei ya Mkaa Video inakuja, kuna Nikumbatie..zote tunaamini zitakuwa na impact tofauti na kazi zilizopita nyuma.” Amefunguka Joh.
Joh na Nikki wa Pili walieleza jinsi ambavyo waliweza kufanikisha kuifikisha Nje ya Box Channel O hadi kupata air time.
“Tulipewa tu connection…kuna mdada alitusaidia tukatafuta connection ya kule akatuma na jamaa wakatutumia form yao tukajibu.” Nikki wa Pili ameeleza.

“Tukatuma kwa email kwa wahusika wanaofanya kazi Channel O, wakaipokea wakaiangalia wakajibu Email kwamba hii kazi tumeipokea na tumeikubali itachezwa hapa Channel O. kwa hiyo I’ts possible, yaani inawezekana kabisa. Cha msingi inatakiwa ianze pale ambapo unafanya video yako mwenyewe kwa sababu wenzetu kule duniani hawashangai tena quality katika hiyo level, kwa sababu quality kila mtu anayo. Lakini ndani ya quality umeweka creativity gani ili mtu aweze kupenda kuitazama kazi yako?” – Joh Makini.

No comments:

Post a Comment