Thursday, February 27, 2014

SERIKALI YATANGAZA AJIRA ZA WAALIMU 2014.

Hatimaye serikali imetangaza ajira mpya za waalimu zilizokuwa
zikisubiriwa kwa hamu. Kwa maelezo zaidi nunua gazeti la uhuru. Majina
bado hayajatolewa, ngoja niwaonjeshe kdg nukuu hii.

"Serikali yatoa nafasi za
walimu zilizokuwa
zikisubiliwa kwa muda
mrefu na wahitimu
waliomaliza vyuo
mbalimbali kwa mwaka 2014, Akiongoea na
waandishi wa habari Mh
Jenista Mhagama
amesema jumla ya
walimu 26750
wamepangwa sehemu mbalimbali nchini,wengi
wakienda katika shule
mpya zilizojengwa na
serikali na kuonya
kwamba yeyote atakae
toroka kituoni na kuchukua pesa za
serikali atachukuliwa
hatua kali za kisheria.
CHANZO MAELEZO LEO
SAA TATU NA NUSU
09:30 (OFISI ZA WIZARA YA ELIMU)"

Wednesday, February 26, 2014

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 27/2/2014..SIASA, MICHEZO NA UDAKU..!

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

HUU NDIO UFAFANUZI KUTOKA BARAZA LA MITIHANI JUU YA ALAMA NA MADARAJA YA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2013

Baraza la Mitihani nchini limetoa ufafanuzi wa alama na madaraja yalivyopangwa kutokana na matokeo ya mtihani wa watahiniwa walioitimu Kidato cha Nne 2012/13 baada ya malalamiko yaliyotokana na mkanganyiko wa utaratibu huo mpya ambao haukuwepo katika miaka ya nyuma.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde amesema utaratibu huo umelenga kupunguza mlundikano wa alama katika kundi moja.

Sasa katika makundi yetu haya saba, kama nilivyotangulia kusema, ni gredi D ndiyo ufaulu. Kama mtahiniwa alipata gredi D na kuendelea, atakuwa amefaulu. Mtahiniwa katika somo,
 akipata gredi D na F, atahesabiwa kuwa ameshindwa somo husika. 

Sasa mtahiniwa huyu anahesabiwa vipi kufaulu kwa ujumla wake mtihani?

Amefanya masomo mbalimbali tunampangaje katika madaraja?

Madaraja ya ufaulu, yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20, kifungu kidogo 1 – 6 cha Kanuni za Mitihani, kinachoelekeza kuwa, Ufaulu katika daraja la I – III upangwe kwa kuzingatia idadi ya alama, yaani points, na ufaulu katika daraja la IV unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini alioupata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au kwa kiwango kisichokuwa chini ya gredi C katika somo moja.

Aidha Dk Msonde amesema sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi kwa kutumia mfumo huo mpya wa madaraja, utatolewa na mamlaka husika, ambapo Kamishana wa Elimu ndiye mwenye mamlaka ya kulitolea ufafanuzi.

----------------

UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013

Ads not by this site
Baraza la Mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe 21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya chini ya ufaulu (pass mark) na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:-

1.  Viwango vya ufaulu (grade ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi mwaka 2012.

Aidha, Kuanzia Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja. Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.

Jedwali Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.

Kundi
Gredi
Alama
Idadi ya Pointi
1
A
75 - 100
1
2
B+
60 - 74
2
3
B
50 - 59
3
4
C
40 - 49
4
5
D
30 - 39
5
6
E
20 - 29
6
7
F
0 -  19
7

Aidha, Idadi ya makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili (12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi (Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.

2.  Kwa kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.

3.  Madaraja ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points) na Ufaulu katika Daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja. Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2.

Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013

Ads not by this site

4. Kwa mujibu wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E na F zitakuwa alama za kufeli.

5. Baraza la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.

Imetolewa Na:

KAIMU KATIBU MTENDAJI

25 Februari, 2014

TIZAMA PICHA ZA YULE ASKOFU GEOR DAVIE HAPA NIKAMA MALAIKA VILE

ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi  kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.
Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.
Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.
Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.
“Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
“Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.
Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka  kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.
“Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud,” alisema Fred Mushi.
Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Monday, February 24, 2014

ALIYETABIRI KUWA MWISHO WA DUNIA NI MWAKA 2000 AMEAGA DUNIA

Space-space-584336 1600 1200 2d4a1
kiongozi wa Kanisa la World Message Last Warning ambaye alitabiri kwamba mwaka 2000 utakuwa mwisho wa dunia, Wilson Bushara (53) amefariki dunia.
Bushara ambaye alivuta vyombo vingi vya habari alipotabiri na kusisitiza kwamba mwisho wa dunia utakuwa Juni 30 mwaka 1999 na kusashawishi waumini wake kuuza mali zao na kununua nafasi zao mbinguni alifariki asubuhi ya jana.

Alitabiri na kusisitiza kwamba dunia itafikia mwisho wake kabla ya kuingia kwa milenia mpya, ambayo ilikuwa ni mwaka 2000.
Hata baada ya tarehe hiyo aliyoitaja kupita bila tukio hilo kutokea, Bushara alikimbilia mafichoni baada ya polisi kuvamia kambo yake ya maombi ya Bukoto iliyokuwa huko kwenye Wilaya ya Luweero Jimbo la Nakaseke Septemba 18, 1999.
Bushara anatambulika kuwa ana ushirikiano na kiongoni mwingine wa kundi la kidini, Joseph Kibwetere ambaye aliwashawishi waumini wake zaidi ya 1000 kujichoma moto kanisani Machi 17, 1999.
Hata hivyo aliamua kukataa kuwa na ushirikiano na Kibwetere pamoja na kuwa na ushahidi wa picha walizopiga kwenye matukio kadhaa wakiwa pamoja.
Bushera pamoja na baadhi ya waumini wake ambao wengi walikuwa wakifanya kazi za kuuza maziwa na uhudumu kwenye hoteli wote walikimbilia wilayani Busia ambapo walijificha baada ya kusikia taarifa kwamba polisi walikuwa wakitaka kuwakamata.
Alioa wake tisa aliokuwa akiishi nao kwa pamoja, mmoja kati yao akiwa binti wa miaka 15. Miaka 10 baadaye, yaani mwaka 2011 Bushara aliibuka na kutabiri kwamba dunia inaelekea kufikia mwisho wake siku za karibuni na kuanza kugawa kadi za mwaliko kwa waumini wake, kwa ajili ya tafrija maalumu ya "karamu ya mwisho" ambazo kila moja iliuzwa kwa Sh23,000 za Uganda.
Aliwaeleza wafuasi wake kwamba ishara za mwisho huo wa dunia ziko wazi ikiwemo miale mikali ya radi na milipuko ya volcano wanayoishuhudia kwa mwaka huo ndiyo uthibitisho kwamba dunia imefikia mwisho. Kwa kusisitiza, aliwahakikishia kwamba wale watakaokuwa wamenunua kadi hizo ndio watakaopata fursa ya 'kunyakuliwa' moja kwa moja kwenda mbinguni na wale ambao hawatakuwa wamezipata, wataishia kwenye moto wa jehanamu.
Kwa wakati huu, Bushara alikuwa makini akikataa kutaja tarehe rasmi ya mwisho huo wa dunia aliokuwa akiutabiri. Bushara amefariki huku akikabiliwa na mashtaka kadhaa mahakamani, ikiwemo kufunguwa kanisa lake ambalo lilipigwa marufuku.
Mei mwaka jana alishtakiwa kwa ulaghai na kuitisha mkusanyiko usiokuwa halali kisheria, kisha kushikiliwa kwenye gereza la Luzira na hatimaye kuachiwa.
CHANZO MWANANCHI

ASKOFU BILIONEA BONGO ATIKISA

Stori: Jelard Lucas
ASKOFU na Nabii George David ‘Geordavie’ wa Kanisa la Geordavie Ministry ‘Ngurumo ya Upako’ lililoko jijini Arusha na Kawe, Dar hivi karibuni alifanya mkutano mkubwa na kutikisa nchi  kwa kuwa na magari ya kifahari na ndege aina ya helikopta ‘chopa’ iliyokuwa ikirandaranda juu ya anga kulinda usalama wake, Uwazi lina ushuhuda wa kutosha.

Katika mkutano huo uliofanyika Karatu mkoani Manyara, mwandishi wetu alishuhudia msafara wa Geordavie ambaye hutoa huduma ya uponyaji kwa njia za miujiza, ukiwavutia watu wengi kwa kuwa ulikuwa na ulinzi mkali ambao haujawahi kutokea.
Mbali ya kuwa na chopa iliyokuwa ikiimarisha ulinzi ambayo ameinunua hivi karibuni, askofu huyo alikuwa na msururu wa magari yenye thamani kubwa yanayomfanya kutajwa kuwa tajiri kuliko maaskofu wengine wanatoa huduma katika makanisa ya kiroho Tanzania.
Akiwa Karatu, mbali na ulinzi binafsi, Geordavie alikuwa akilindwa na askari wa jeshi la polisi, askari kanzu, Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wale wa usalama barabarani.
Mbali na askari hao wa serikali ambao wamekuwa wakimlinda kila anapofanya mikutano yake, pia Geordavie analindwa na askari wake binafsi hali iliyowafanya baadhi ya watu kuamini kuwa ulinzi wake ni kama ule wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete ‘JK’.
“Sijawahi kumuona JK akilindwa na chopa lakini mtumishi wa Mungu Geordavie analindwa na ndege katika msafara wake! Hii ni mara yangu ya kwanza kuona,” alisema muumini mmoja ambaye hakupenda kutajwa gazetini.
Hata hivyo, baadhi ya watu walikuwa wakihoji utajiri wa askofu huyo kutokana na fedha nyingi anazozitumia anapofanya mikutano katika sehemu mbalimbali jijini Arusha.
“Tunajua kuwa ni tajiri, lakini anapata wapi fedha za kutumia hivi?” alihoji muumini aliyejitambulisha kwa jina moja la Julius ambaye naye alihudhuria mkutano wa askofu huyo anayetumia kaulimbiu ya Ngurumo ya Upako katika kutoa huduma yake.
Pia, waumini wengine walilalamikia ugumu wanaoupata wanapotaka  kumuona mtumishi huyo wa Mungu kutokana na ulinzi mkali anaopewa.
“Kila mtu alitamani kumuona mtumishi wa Mungu lakini haikuwezekana kutokana na ulinzi wake kuwa mkali, utajiri wake hakuna mfano, hata kule nyumbani kwake Arusha, anaishi kama Mfalme Daud,” alisema Fred Mushi.
Gazeti hili lilimsaka Askofu na Nabii Geordavie kwa lengo la kutaka kujua sababu ya kuwa na ulinzi mkali na kutumia magari ya kifahari ikiwemo chopa katika mikutano anayoifanya lakini simu yake iliita bila kupokelewa.

Friday, February 21, 2014

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2013 HAYA HAPA