Baraza la Mitihani nchini limetoa ufafanuzi wa alama na madaraja yalivyopangwa kutokana na matokeo ya mtihani wa watahiniwa walioitimu Kidato cha Nne 2012/13 baada ya malalamiko yaliyotokana na mkanganyiko wa utaratibu huo mpya ambao haukuwepo katika miaka ya nyuma.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam
leo, Kaimu Mtendaji wa Baraza hilo Dk Charles Msonde amesema utaratibu
huo umelenga kupunguza mlundikano wa alama katika kundi moja.
Sasa katika makundi yetu haya saba, kama nilivyotangulia kusema, ni gredi D ndiyo ufaulu. Kama mtahiniwa alipata gredi D na kuendelea, atakuwa amefaulu. Mtahiniwa katika somo,
akipata gredi D na F, atahesabiwa kuwa ameshindwa somo husika.
Sasa mtahiniwa huyu anahesabiwa vipi kufaulu kwa ujumla wake mtihani?
Amefanya masomo mbalimbali tunampangaje katika madaraja?
Madaraja ya ufaulu, yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20, kifungu kidogo 1 – 6 cha Kanuni za Mitihani, kinachoelekeza kuwa, Ufaulu katika daraja la I – III upangwe kwa kuzingatia idadi ya alama, yaani points, na ufaulu katika daraja la IV unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini alioupata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili au kwa kiwango kisichokuwa chini ya gredi C katika somo moja.
Aidha Dk Msonde
amesema sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi kwa kutumia mfumo huo
mpya wa madaraja, utatolewa na mamlaka husika, ambapo Kamishana wa Elimu
ndiye mwenye mamlaka ya kulitolea ufafanuzi.
----------------
UFAFANUZI WA MASWALI MBALIMBALI YA WADAU WA ELIMU KUHUSU MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2013
Ads not by this site
Baraza la Mitihani la Tanzania
lilitangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013 tarehe
21/02/2014. Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Baraza limekuwa
likipokea maswali mbalimbali yanayoashiria kuwa baadhi ya wadau wa elimu
hawakuelewa vizuri kuhusu Viwango vya Ufaulu (grade ranges), alama ya
chini ya ufaulu (pass mark)
na Ufaulu wa jumla wa mtahiniwa (overall performance). Baraza la
Mitihani linapenda kutoa ufafanuzi katika mambo hayo kama ifuatavyo:-
1. Viwango vya ufaulu (grade
ranges) ni makundi ya alama yanayopangwa ili kuwaweka pamoja watahiniwa
wenye uwezo unaofanana katika somo husika na kuwatofautisha na
watahiniwa waliopo katika kundi jingine. Makundi haya hupangwa ili
kuwawezesha wadau kutambua namna watahiniwa walivyotawanyika katika
viwango mbalimbali vya umahiri wa somo husika. Baraza la Mitihani la
Tanzania, limekuwa likitumia makundi Matano (5) kwa kipindi kirefu hadi
mwaka 2012.
Aidha, Kuanzia
Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) 2013, Baraza limeanza kutumia utaratibu
wa Makundi Saba (7) ambayo ni A, B+, B, C, D, E na F. Utaratibu huu
umelenga kupunguza mlundikano mkubwa wa alama katika kundi moja.
Mgawanyo wa makundi hayo ni kama inavyoonekana kwenye Jedwali la 1.
Jedwali Na 1: Viwango vya ufaulu vilivyotumika katika Matokeo ya CSEE 2013.
Kundi
|
Gredi
|
Alama
|
Idadi ya Pointi
|
1
|
A
|
75 - 100
|
1
|
2
|
B+
|
60 - 74
|
2
|
3
|
B
|
50 - 59
|
3
|
4
|
C
|
40 - 49
|
4
|
5
|
D
|
30 - 39
|
5
|
6
|
E
|
20 - 29
|
6
|
7
|
F
|
0 - 19
|
7
|
Aidha, Idadi ya
makundi ya ufaulu hutofautiana kati ya nchi na nchi kulingana na
mahitaji ya nchi husika. Kwa mfano; Kenya wana makundi Kumi na mbili
(12), Malawi Tisa (9), Uganda Tisa (9), Nchi za Afrika magharibi
(Nigeria, Ghana, Siera Leone na Liberia) makundi Tisa.
2. Kwa
kuzingatia viwango vya ufaulu vilivyoainishwa katika makundi saba
yaliyopo kwenye Jedwali na 1, kiwango cha chini cha ufaulu ni gredi D na
kiwango cha juu cha ufaulu ni Gredi A. Mtahiniwa atakuwa amefaulu somo
husika iwapo atapata gredi D na kuendelea. Aidha, mtahiniwa aliyepata
gredi E na F atakuwa hajafaulu somo husika.
3. Madaraja
ya ufaulu yamepangwa kwa mujibu wa kifungu cha 20 (1)-(6) cha Kanuni za
Mitihani kinachoelekeza kuwa Ufaulu katika daraja la Kwanza hadi la
Tatu upangwe kwa kuzingatia jumla ya alama (Points)
na Ufaulu katika Daraja la Nne unapangwa kwa kuzingatia ufaulu wa chini
aliopata mtahiniwa ambao ni gredi D katika masomo yasiyopungua mawili
au ufaulu kwa kiwango kisichokuwa chini ya Gredi C katika somo moja.
Hivyo, madaraja yaliyotumika ni kama yanavyoonekana kwenye Jedwali la 2.
Jedwali 2: Madaraja yaliyotumika katika CSEE 2013
Ads not by this site
4. Kwa mujibu
wa Kanuni za Mitihani, ufaulu wa somo katika Gredi A hadi C utakuwa ni
ufaulu wa “Credit” na Gredi D itahesabika kuwa ni “pass”. Aidha Gredi E
na F zitakuwa alama za kufeli.
5. Baraza
la mitihani la Tanzania linapenda kutoa taarifa kwamba ufafanuzi wa
sifa za kujiunga na mafunzo katika ngazi mbalimbali kwa kutumia mfumo
huu mpya wa madaraja utatolewa na mamlaka husika ambapo Kamishna wa
Elimu atalitolea ufafanuzi zaidi.
Imetolewa Na:
KAIMU KATIBU MTENDAJI
25 Februari, 2014
No comments:
Post a Comment