Thursday, January 2, 2014

TASWIRA YA NYUMBANI KWA MAREHEMU DR MGIMWA ALIPOZALIWA.... ALIKUWA NI KIONGOZI ASIYEPENDA KUJILIMBIKIZIA MALI....


Hapa  ndipo  nyumbani  alipozaliwa na alipokuwa akiishi  aliyekuwa  waziri  wa fedha na mbunge wa  jimbo la Kalenga Dr Wiliam Mgimwa na ndipo atazikwa hapa


Hii ndio nyumba ya  waziri wa fedha  Dr Wiliam Mgimwa  iliyopo jimboni Kalenga ambako ndipo alipozaliwa ikiwa na bendera   ikipepea  nusu mlingoti

Hii  ni  nyumba anayoishi mama yake  ambayo  ipo  jirani na yake

Wanachama wa CCM wakibadilisha  bendera  nyumbani kwa aliyekuwa waziri wa fedha  jioni ya  leo .usikose  kujua habari  zaidi baadae juu ya maisha ya  waziri Dr Mgimwa.

Angalia hapa picha hapa chini  Sehemu atakapozikwa marehemu dk William Mgimwa kijijini Magunga

Katibu wa mbunge Dr Wiliam Mgimwa Bw Martine Simangwa akiwaonyesha viongozi  wa  CCM eneo ambalo waziri Mgimwa atazikwa  katika  kijiji  cha Magunga kata  ya Maboga  jimbo la Kalenga. No comments:

Post a Comment