Saturday, December 28, 2013

HUKO TARIME: MKE ACHARANGWA MAPANGA, HAWARA ATAJWA KUWA NDIO CHANZO...!




Stori: Timoth Itembe, TARIME
MAMA mmoja mkazi wa Ronsoti, Kata ya Nyamisangura, wilayani hapa, Eliza Marwa,28, hivi karibuni amenusurika kuuawa na mumewe, baada ya majirani kufika kumuokoa kutokana na kukatwakatwa mapanga.



Mariamu akiugulia maumivu.

Mama huyo aliliambia gazeti hili akiwa katika Hospitali ya Wilaya Bomani, Tarime kuwa mume wake Marwa Ogora alimkatakata mapanga baada ya
kumtuhumu kuwa akikwenda kwa hawara yake badala ya kwenda kwenye mazishi ya mjomba wake huko Bunchari.


Akifafanua zaidi, Eliza alikuwa na haya ya kusema: ‘’Mjomba alifariki na mazishi yake yalifanyika Desemba, kumi na sita mwaka huu ambapo nilihudhuria baada ya kumwarifu mume wangu kuwa nitahudhuria lakini alinijibu kuwa hakuwa na fedha za kunipa ili niende kwenye mazishi.

“Nilichukua jukumu la kwenda kwa kutumia nauli yangu kwa kuwa muda huo mume wangu alikuwa kazini na baada ya mazishi kesho yake asubuhi Desemba kumi na saba mwaka huu nilirudi nyumbani na kumkuta mume wangu ambaye alianza kunipiga kwa mpini wa jembe kisha panga akidai kuwa sikuwa nimeenda kwenye mazishi badala yake nilikuwa nimeenda kwa mpenzi wangu.

“Alinishambulia sehemu mbalimbali za mwili hususani kichwani, kidogo anitoe ubongo, wasingekuwa majirani kuniokoa baada ya kupiga yowe naamini angeniua kwani hivi sasa siwezi hata kuamka na masikio yameziba, miguu ina ganzi, siwezi kutembea.

“Mume wangu Ogora amekuwa akinipiga mara kwa mara lakini kutokana na watoto tuliozaa naye nimekuwa nikivumilia mateso, naogopa kuondoka na kuacha watoto walelewa na mama wa kambo,”alidai mama huyo.

Ogora hakupatikana kuzungumzia tukio hilo kwani anasakwa na dola na afisa mmoja wa polisi wilayani hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema wanaendelea kumtafuta mtuhumiwa. Naye daktari wa hospitali aliyolazwa mama huyo, Nega Malico alikiri kumpokea mgonjwa huyo.

No comments:

Post a Comment