Saturday, January 11, 2014

MWANDISHI FORTUNATA RINGO AFARIKI DUNIAFortunata akiwa katika mafunzo ya MCT ya maadili Manyara
Blogu hii saa moja iliyopita imepokea habari za kusikitishwa kwamba mwandishi wa habari wa Habarileo Manyara Fortuinata Ringo amefariki dunia.

kwa mujibu wa ndugu yake Glad mwandishi huyo amefariki dunia leo asubuhi wakati akikimbizwa hospitalini.

Mwandishi huyo aliyezaliwa septemba 25,1980 jijini Dar es Salaam na kusomea shule ya msingi Ubungo NHC ba kusoma sekondari ya  Aya iliyoko Kondoa amefariki wakati akisubiri tiketi ya kwenda India kwa matibabu.

Fortunata ambaye alipata reaction ya dawa ya malaria 2011 na kutibiwa Muhimbili alikuwa amekamilisha mchakato wa kupelekwa india kutibiwa tatizo linaloitwa kitaalamu kama SLE.

  Kwa mujibu wa dada yake Glad, mipango ya mazishi inafanyika na msiba upo kwa wazazi wake Ubungo Kibangu karibu na stendi ya Makuka.

Mungu ametoa Mungu ametwaa jina la bwana lihimidiwe AMINA

No comments:

Post a Comment