Friday, January 24, 2014

MSANII WA BONGO MUVI ANYWA SUMU KISA PENZI LA MDOGO WA KANUMBA....SOMA ZAIDI HAPA....

 

Msanii chipukizi wa filamu wa Kundi la Mwamba Arts, Mariam Glant.
MSANII chipukizi wa filamu wa Kundi la Mwamba Arts, Mariam Glant (20) amenusurika kifo baada ya kunywa sumu kisa kikidaiwa kuwa ni penzi la kijana aliyejifanya mdogo wa Kanumba anayejulikana kwa jina moja la Chief.

Akizungumza na paparazi wetu sosi wa karibu na msanii huyo alisema siku ya tukio, Mariam alikuwa nyumbani kwa rafiki yake wa kike maeneo ya Mbezi Mwisho, jijini Dar ambapo rafiki yake huyo alitoka kidogo na kumuacha peke yake nyumbani hapo. 

Sosi huyo alisema baada ya muda mfupi alitumiwa ujumbe mfupi wa maneno kutoka kwa Mariam ukisema ‘mimi ndiyo nakufa hivyo nimekunywa sumu.’ 

Baada ya rafiki huyo kupata ujumbe huo, alirudi nyumbani haraka na kumkuta Mariamu akiwa amezimia huku akitokwa na mapovu mdomoni ambapo kwa kushirikiana na wasamaria wema walimchukua na kumkimbiza kituo cha polisi kuchukua PF3 na kumpeleka hospitali ya tumbi ambapo alipatiwa matibabu.

Akielezea kwa uchungu baada ya kupata ahueni, Mariam alisema yeye na mpenzi wake huyo waligombana siku chache kabla hajachukua uamuzi wa kunywa sumu.
“Sababu kubwa iliyonifanya ninywe sumu ni huyo mwanaume kwa sababu kwanza alinidanganya yeye ni mdogo wake Kanumba na nikiwa naye kimapenzi atanitoa kisanaa na nitakuwa maarufu lakini baada ya kuingia kwenye uhusiano hakunisaidia chochote zaidi nilikuja kugundua kwamba hana hata undugu na Kanumba tukagombana,” alisema Mariam aliyeng’ara katika sinema za Mwanamipango Comedi, Gods Kingdom na M23.

No comments:

Post a Comment