Wednesday, January 29, 2014

CHIEF KIUMBE ASEMA SABABU ZA KUMNUNULIA DIAMOND GARI LA KIFAHARI



(AUDIO) CHIEF KIUMBE AKIELEZEA SABABU ZA MISAADA YAKE KWA WASANII NA SEHEMU MBALIMBALI BONGO. Kwa muda mrefu Tanzania jina la mfanya biashara maarufu, Chifu Kiumbe limekuwa intro ama outro kwenye nyimbo nyingi za wasanii wa bongo flava na muziki wa dansi nchini kutokana na misaada mbalimbali anayoitoa kwa wasanii hao.
Maswali mengi yamekuwa yakiulizwa kwa muda mrefu bila majibu sahihi kutoka kwa mhusika mwenyewe ‘kwa nini hutoa misaada hiyo na yeye anafaidika na nini?
Chief Kiumbe ambaye jina lake halisi ni Muhammed Abdallah Kiumbe, amefunguka exclusively kupitia kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm katika ‘Exclusive Friday’ ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwake kufanya mahojiano na kituo cha radio hapa nchini.
Akifanya mahojiano na Samira, Fadhili Haule na Erick, Chifu Kiumbe aliweka wazi kuwa yeye ndiye aliyemnunulia Diamond Platinumz gari aina ya Toyota Land Cruiser V8. Na kwamba alilinunua kwa $100,000 na ushuru alilipia takribani Million 85 za Tanzania.
“Kuna rafiki yangu hapa mmoja magazeti yanamuandika andika yanasema ‘mzee wa kuloga, japokuwa…rafiki yangu Diamond. Naseeb ni rafiki yangu, swaiba wangu na kipenzi changu. Kuna gari moja kubwa sana analitembelea sasa hivi, zuri sana…najua mnajua lakini mnataka tu nizungumze.” Chief Kiumbe amefunguka kwenye kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm.
“Ni gari ya thamani, kwa sababu nafikiri…nililinunua $100,000 na ushuru wake kama million 85 (za Tanzania), ukijumlisha inakuja kama ‘two forty five’, ni kama million 245.” Ameeleza.
Akielezea sababu za kumnunulia Diamond gari hilo, amesisitiza kuwa ni rafiki yake wa karibu na kwamba kuna mambo ya ndani wanayafahamu wao wawili kama marafiki, “aah..ni mshikaji wangu Diamond, tumeongea naye kiundaniundani mimi na yeye.”
 
Alipoulizwa kama kuna mkataba wowote kati yake na Diamond, Chief Kiumbe alifunguka, “hakuna mkataba…nimekwambia ni rafiki yangu na swaiba wangu kwa hiyo tunayajua wenyewe chini ya kapeti.”
Hata hivyo, amekiri kuwa Diamond ni msanii mwenye pesa nyingi kwa kiwango chake na kwamba anafanya vizuri kwenye muziki wake, na pia akawashauri wasanii wengine waige mfano wake ili waweze kufanikiwa pia zaidi katika kazi zao za muziki kama alivyofanya Diamond Platinumz.
Akizungumzia kuhusu kile anachokipata kwa wasanii kufuatia misaada mbalimbali mikubwa anayowapa, amesema kuwa yeye hutoa bure na hategemei kurudishiwa. Ametoa mfano kuwa kwa kipato cha wasanii wa Tanzania hakuna ambacho watampa.
“Nadhani dada unaweza ukaelewa maana ya… (akataja neno la kiarab lenye maana ya kutoa msaada) kutoa msaada bure. Sasa ngoja nikuulize swali sawa, mfano mimi sawa, Diamond akipiga show yake ama Tunda akipiga show yake sawa…sasa atanipa nini?” ameeleza.
Lakini hakuna kitu cha bure ‘there is no free lunch in America’, Chief Kiumbe ama The Big Boss kama wanavyomuita waasanii ameeleza kidogo anachokipata kutoka kwa wasanii hao.
“Yeye anakuja kwangu, shukurani kwangu kwamba labda ‘swaiba wangu wewe una party’, nina birthday ya mtoto wangu Halima, au mke wangu birthday yake mama Rajab. Kwa hiyo njoo Diamond unipigie birthday yangu ya watoto wangu tufurahi hapa nyumbani. Basi Tunda njoo ukamue hapa, Shetta njoo ukamue hapa.”
Mfanyabiashara huyo ambaye ameeleza kuwa ni mmiliki wa bendi ya Extra Bongo lakini mafao yote anayachukua swaiba wake Ally Choki ambaye amemtaja kama mtu aliyelitangaza kwa mara ya kwanza jina lake Tanzania, amesema amewapa mkataba wasanii wote wanaohusika na bendi ya Extra Bongo ambao unampa msanii nyumba na gari ambavyo anavitumikia katika kipindi cha miaka mitano katika bendi hiyo.
Ameongeza kuwa, mbali na kuwasaidia wasanii hujihusisha pia na kuisaidia jamii na kupitia huko hapendi kujitangaza. Ametoa mfano kuwa aliisapoti kwa kiasi kikubwa ziara ya Diamond alipotembelea vituo vya watoto yatima.
Kipindi cha Sun Rise cha 100.5 Times Fm huendeshwa na Samira, Fredwaa, Fadhili Haule na Eric kila siku za wiki kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa tatu kamili. Unaweza kusikiliza online kupitia tovuti hii. Bofya sehemu iliyoandikwa ‘Listen’.
Sikiliza hapa kipande cha mahojiano hayo, na endelea kutembelea www.timesfm.co.tz utamfahamu vizuri Chief Kiumbe na biashara anazofanya na uhusiano wake na Raila Odinga wa Kenya.
@Times fm

No comments:

Post a Comment