Tuesday, December 17, 2013

SUMATRA YASITISHA LESENI ZA USAFIRISHAJI KWA MABASI YA BURUDANI, POLEPOLE CLASSIC NA OSAKA ROYAL CLASS ..

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUSITISHA LESENI ZA USAFIRISHAJI KWA MABASI YANAYOMILIKIWA NA KAMPUNI ZA OSAKA ROYAL CLASS, POLEPOLE CLASSIC NA BURHAN BUS SERVICES

Hivi karibuni mabasi yanayomilikiwa na kampuni za Osaka Class, Polepole Classic na Burhan Bus Services yalihusika katika ajali zilizotokea katika maeneo na siku tofauti ambapo watu walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa. 
  
Kutokana na hali hiyo Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imechukua hatua kwa wahusika kama ifuatavyo:

1.      Kampuni ya Osaka Royal Class 
Mnamo tarehe 10/12/2013, Basi la Kampuni ya Osaka Royal Class lenye namba ya usajili T819BYL lililokuwa likiendeshwa na Bwana Emmanuel Semkamba kutokea Arusha kuelekea Dar es Salaam, lilipata ajali maeneo ya Kirinjiko katika Wilaya ya Same Mkoani Kirimanjaro. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watatu (03) na majeruhi thelathini na watatu (33).
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kushindwa 
kulimudu baada ya kupata hitilafu ya kiufundi kutokana na mwendo kasi.
Kwa kuzingatia Kifungu Namba 15 cha Sheria ya SUMATRA na pia Kanuni Namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma  za Mwaka 2008, Mamlaka imeamua kusitisha leseni za usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na kampuni ya Osaka Royal Class yenye namba za usajili T819BYL, T417 AAG, T852 AUL, T206 CJZ, T201 CJZ, T437 BJK na T852 AUL.
Leseni za Usafirishaji kwa magari yaliyotajwa hapo juu zinasitishwa hadi hapo yafuatayo yatakapotekelezwa:
 1. Kuhakikisha kuwa mabasi ya Kampuni yaliyoorodheshwa hapo juu yanakaguliwa na Mkaguzi kutoka Jeshi la Polisi na kuthibitisha iwapo yanakidhi viwango vya ufundi na usalama.
 2. Kuwasilisha picha (passport size) ya dereva aliyesababisha ajali hiyo pamoja na nakala ya leseni yake ya udereva.
 3. Madereva wa mabasi yaliyotajwa hapo juu wajaribiwe na Jeshi la Polisi kwa lengo la kujiridhisha kama wana sifa za kuendesha mabasi.
 4. Kuwasilisha kwa maandishi mpango utakaotumiwa na Kampuni katika kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva wake.
2. Kampuni ya Polepole Classic 
Mnamo tarehe 8/12/2013, Basi la Kampuni ya Polepole Classic lenye namba za usajili T898BKN likiendeshwa na Stephano Pangawazi  kutokea Moshi kuelekea Babati, lilipata ajali maeneo ya Kijiji cha Machangarawe katika  Wilaya ya Babati Mkoani Manyara. Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu watano(5) na majeruhi thelathini na wawili (32).
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa basi hilo kushindwa kuchukua tahadhari wakati akiendesha basi usiku kulikopelekea kuligonga trekta lililokuwa likiendeshwa barabarani.
Kwa kuzingatia Kifungu Namba 15 cha Sheria ya SUMATRA na pia Kanuni Namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma  za Mwaka 2008, Mamlaka imeamua kusitisha leseni za usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na Kampuni ya Polepole Classic katika njia ya Moshi-Babati yenye namba za usajili T898 BKN, T267AZL na T212BLZ.
Leseni za Usafirishaji kwa magari yaliyotajwa hapo juu zinasitishwa hadi hapo yafuatayo yatakapotekelezwa:
 1. Kuhakikisha kuwa mabasi ya Kampuni yaliyoorodheshwa hapo juu yanakaguliwa na Mkaguzi kutoka Jeshi la Polisi na kuthibitisha iwapo yanakidhi viwango vya ufundi na usalama.
 2. Kuwasilisha picha (passport size) ya dereva aliyesababisha ajali hiyo pamoja na nakala ya leseni yake ya udereva.
 3. Madereva wa mabasi yaliyotajwa hapo juu wajaribiwe na Jeshi la Polisi kwa lengo la kujiridhisha kama wana sifa za kuendesha mabasi.
 4. Kuwasilisha kwa maandishi mpango utakaotumiwa na Kampuni katika kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva wake.
3. Kampuni ya Burdani Bus Service 
Mnamo tarehe 12/12/2013, basi lako lenye namba za usajili T610ATR lililokuwa likiendeshwa na Bwana Ruta Kwadahel likitokea Korogwe kuelekea Dar es Salaam, katika barabara ya Arusha- Dar es Salaam lilipata ajali maeneo ya Kijiji cha Taula, Wilaya ya Handeni, Mkoani Tanga. Ajali hiyo ilisababisha  vifo vya watu 12 na majeruhi 93.
Taarifa za awali kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi, uzembe wa dereva wa basi hilo  na kujaza abiria kupita kiasi.
Kwa kuzingatia Kifungu Namba 15 cha Sheria ya SUMATRA na pia Kanuni Namba 22 ya Kanuni za Ufundi na Usalama na Ubora wa Huduma  za Mwaka 2008, Mamlaka imeamua kusitisha leseni za usafirishaji kwa mabasi yanayomilikiwa na kampuni hiyo yenye namba za usajili T158BXG, T610ATR, T572BXJ, T994AGD, na T607ATR.
Leseni za Usafirishaji kwa magari yaliyotajwa hapo juu zinasitishwa hadi hapo yafuatayo yatakapotekelezwa:
 1. Kuhakikisha kuwa mabasi ya Kampuni hiyo yaliyoorodheshwa hapo juu yanakaguliwa na Mkaguzi kutoka Jeshi la Polisi na kuthibitisha iwapo yanakidhi viwango vya ufundi na usalama.
 2. Kuwasilisha picha (passport size) ya dereva aliyesababisha ajali hiyo pamoja na nakala ya leseni yake ya udereva.
 3. Madereva wa mabasi yaliyotajwa hapo juu wajaribiwe na Jeshi la Polisi kwa lengo la kujiridhisha kama wana sifa za kuendesha mabasi.
 4. Kuwasilisha kwa maandishi mpango utakaotumiwa na Kampuni katika kudhibiti ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva wake.
Imetolewa na:
David Mziray
Meneja Mawasiliano
SUMATRA

No comments:

Post a Comment