Wednesday, December 11, 2013

MAPENZI NOMA SANA:MDADA APIGWA NA KUKATWA VIDOLE BAADA FUMANIZI..! SAMAHANI KWA PICHA INATISHA 
Mwanamke mmoja apigwa vibaya na mume wake hadi kukatwa vidole baada Mumewe kugundua kuwa anamsaliti, Tukio hilo lilitokea majira ya jioni jamaa huyo aliporudi kazini na kumkosa mke wake baada ya kumpigia simu alisema yuko kwa rafiki yake, jamaa aliwasha gari na kufika hadi kwa huyo rafiki yake, alipofika alimpigia tena simu na kumuambia nimefika mke wangu niko hapa nje , mwanamke alisema kuwa wametoka kidogo yeye na huyo rafiki yake ila watarudi muda sio mrefu, jamaa alimuuliza mke wake mko wapi ili niwafuate huko sasa hivi mwanamke alieleza kwamba wako bekari wanaangalia nini cha kununua, jamaa akamuambia mke wake nisubiri hapo hapo nakuja usiondoke,..  
alipofika eneo hilo aliloelekezwa hakukuwa na bakery alijaribu kuulizia hakufanikiwa kupata bekari, alimpigia tena mke wake simu na kumuuliza mbona maeneo haya hakuna bakery? mwanamke akajibu nimeshatoka huko niko njiani sasa hivi nakaribia kwa rafiki yangu. 
Jamaa alirudi tena kwa hasira na kufika pale kwa huyo rafiki yake. akamkuta mke wake yuko pale akamuomba warudi nyumbani. Walivyofika nyumbani jamaa akamuuliza mke wake ulikuwa wapi? mwanamke akajibu kwa rafiki yangu, huku akiogopa na kuonekana ana wasi wasi. 
Alichukua simu yake meseji ya kwanza aliyokutana nayo ni ya mwanaume ikisema "nipo kwangu mpenzi mbona hufiki" jamaa alianza kushusha kipigo cha mbwa mwizi hadi kufikia kumkata mwanamke huyo vidole na kumuumiza vibaya. 

No comments:

Post a Comment