Tuesday, November 12, 2013

JESHI LA POLISI WASHUTUMIWA KUCHUKUA LAKI MBILI KILA WIKI KWA WAUZA GONGO ILI WASIWAKAMATE NA WAWAACHE WAENDELEE NA BIHASHARA YAO MKOANI M


Baadhi ya Raia wa Kitanzania katika kijiji cha Riroda Wilayani Babati Mkoani Manyara wakijipatia Mvinyo asilia maarufu kama (Gongo) unaotengenezwa hapa hapa kwetu, mchena kweupe bila kuhofia askari, MAASINDA BLOG ilishuhudia watu hao wakilewa na kudai kuwa hakuna Askari anayefika maeneo hayo.
 
 Mwandishi wa MAASINDA alipotaka kujua kama Polisi wanafika maeneo hayo aliambiwa kuwa, huwa wanafika kila mwezi na kuchukua hela kidogo ili wasiwafikishe kituoni na wawaache waendelee na Bihashara hiyo.

"Kwa kawaida Askari wanafikaga hapa kila wiki kuchukua laki mbili yao ya kuwafunga Midomo, na ndio maana una waona watu wanakunywa hii kitu haramu bila woga", alisema moja ya Mlevi wa Gongo ambaye hakutaka jina lake liandikwe Mtandaoni.

MAASINDA ilimtafuta Kamanda wa Polisi  Mkoani Manyara lakini hakupatikana baada ya kupigiwa simu yake ya Kiganjani na kutokuita ikiwa imezimwa

Hapa wakipata Gongo kwa kushirikiana ambapo kikombe hicho kidogo kinauzwa kwa shilingi 500 tu.

                                                                                  
Hapa wakisubiria pombe Ipande kichwani

 
Baada ya Kunywa raha yake ndio hii.

No comments:

Post a Comment