Saturday, November 23, 2013

HII NDIYO TWEET YA KWANZA YA ZITTO TANGU AVULIWE VYEO VYOTE NDANI YA CHADEMA

tweet 111
1Hiyo hapo juu ndio tweet yenyewe na ukitazama hapo chini, Zitto Kabwe amebadilisha pia baadhi ya vitu kwenye profile yake kama unavyoona, hii hapa chini ni ya zamani.Profile yake ya sasa ni hii hapa chini…
3

2
November 22 2013 Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kilitangaza kumvua nyadhifa zote Naibu Katibu mkuu wake Zitto Kabwe ambae ni mbunge wa Kigoma Kaskazini ambapo Mwanasheria mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu kwenye makao makuu ya chama hicho, amesema Zitto na wenzake watatu wamebainika kukihujumu chama kwa kuanzisha kitu kinaitwa Mkakati 2013 kinacholenga kukisambaratisha chama hicho ili kuwaondoa madarakani Mwenyekiti na Katibu mkuu wake.
Nyadhifa alizovuliwa ni Unaibu katibu mkuu pamoja na Naibu kiongozi wa upinzani bungeni.

No comments:

Post a Comment