Thursday, November 28, 2013

AMA KWELI PENZI NI KIKOHOZI: RAY, CHUCHU HANS LAIVU..!!! CHEKI HAPA


KAMA WEWE BADO HUJAJIUNGA NASI, UNAWEZA KUJIUNGA HAPA MOJA KWA MOJA ONLINE <<> :

Stori: Gladness Mallya
AMA kweli penzi ni kikohozi kulificha huwezi! Hatimaye uliokuwa uhusiano wa chini kwa chini wa nyota wawili wa sinema za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ na Chuchu Hans, siyo siri tena baada ya wahusika hao wakuu kujiachia ‘live’, Ijumaa limeshiba.
Ray na Chuchu Hans wakiwa katika pozi la kimahaba.

KIMAHABA ZAIDI
Ishu hiyo ilitokea mapema wiki hii ambapo Chuchu alitundika picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Ray chumbani kimahaba.
Kufuatia tukio hilo kuliibuka gumzo kubwa na kulifanya jambo hilo kuwa ndiyo habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa filamu za Kibongo.

Katika picha hiyo, Chuchu anayetumia jina la Chukichuku kwenye Instagram aliambatanisha na maneno yaliyosomeka ‘Me n U’ akimaanisha yeye na Ray hivyo kutoa fursa kwa mashabiki wao kusema chochote.
Kwa mujibu wa mashabiki hao, Ray na Chuchu kwa sasa ndiyo love bird au ‘maua’ yanayopendezesha tasnia hiyo.
“Mmependezaaa…mapenzi waziwazi,” ilisomeka komenti ya mmoja wa mashabiki hao.

“Nilikuwa simuelewi Ray lakini hapa nimemsoma. Wamependeza sana,” ilisomeka komenti nyingine iliyoungwa mkono na mashabiki wengi kwa kupata ‘likes’ nyingi.
Mwingine aliandika: “Sasa walichokuwa wanagombea Mainda (Ruth Suka) na Johari (Blandina Chagula) kipo wapi? Ona sasa wamekosa wote… hahahaaa… wawaache miaka isiyohesabika.”

HAKUNA KIFICHO TENA
Katika kunogesha mambo, baadaye Chuchu aliweka picha ya Ray akimsifia jambo lililodhihirisha kuwa kwa sasa hawafanyi tena kificho kama miezi kadhaa iliyopita.
Habari za chini ya kapeti kutoka kwa wasanii wenzao wanaokuwa nao lokesheni zilieleza kuwa wawili hao wamekuwa wakionesha waziwazi kuwa wao ni item (kitu kimoja).

“Kuna siku tulikuwa tuna-shoot maeneo ya Sinza-Mori (Dar), yaani ungewaona wala usingeuliza maana kama hujui kusoma, ungeangalia hata picha. Yaani mapenzi kama njiwa!
“Sasa hivi ndiyo uhusiano ambao upo ‘hoti’ kwenye tasnia yetu, sema ndiyo hivyo wenyewe walikuwa hawapendi ijulikane lakini naona wameshindwa kuendelea kujificha,” alisema mwigizaji huyo kwa sharti la kutotajwa gazetini.

CHUCHU ATAKA WASIINGILIWE
Baada ya kujikusanyia data, Ijumaa lilimtafuta Chuchu akiwa mmoja wa wahusika wakuu ambapo alipopatikana alikuwa na haya ya kusema: “Hayo ni mambo yetu binafsi, naomba tusiingiliwe katika mambo yetu.”
Ijumaa: Chuchu wewe ni kioo cha jamii na mashabiki wako wanataka kujua ukweli juu ya uhusiano wako na Ray. Unalizungumziaje hilo?

Chuchu: Weweee…sikia! Nimeshasema sitaki mtu aniingilie mambo yangu. Kwani mnataka nini nyiye?
Ijumaa: Je, hiyo picha mliyopiga chumbani ni hotelini au nyumbani?
Chuchu: Siwezi kukuelezea tumepiga wapi, iwe hotelini au nyumbani haiwahusu, naomba mniache jamani mbona hivyo? Kwani vipi? (kisha akakata simu).

KAKA MKUBWA VIPI?
Jitihada za kumpata Ray ‘Kaka Mkubwa’ katika tasnia ya filamu za Kibongo ili kupata neno lake juu ya ishu hiyo ziligonga mwamba baada ya simu yake ya kiganjani kuita bila kupokelewa na hata alipofuatwa ofisini kwake, RJ Productions pale Sinza-Mori, Dar hakupatikana.

KABLA YA PICHA
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai mazito kuwa Ray na Chuchu wanatoka lakini habari hizo zilikosa mashiko kwa kuwa hakukuwa na ushahidi wowote.
Ilidaiwa kuwa hata ile vita ya hivi karibuni ambapo Johari na Chuchu walizichapa kavukavu ilitokana na kugombea penzi la Ray.

JOHARI ASARENDA
Hata hivyo, baadaye Johari alinyoosha mikono kuashiria ‘kusarenda’ na kumwachia Chuchu atawale ulingo ambao ulimshinda pia Mainda.
Ilidaiwa kuwa katika kutekeleza kile walichokiita mpango wa siri, Chuchu na Ray waliunda kampuni yao na kuipa jina la kolabo la Chura wakimaanisha Chuchu na Ray.

TATIZO KUBWA
Wakati hayo yakiendelea, taarifa rasmi ni kwamba bado Chuchu ni mke wa ndoa wa bosi wa Kampuni ya 2 Eyez Productions, Frank Mtao anayeishi ughaibuni huko Australia akiwa ni mwenyekiti wa Wabongo waishio pande hizo.

Mbali na kuwa mke wa mtu, pia Chuchu ni mama wa watoto wawili hivyo uhusiano wake tata na Ray unalenga kuzalisha tatizo kubwa kwenye ndoa ya Chuchu ikiwa ni miezi kadhaa tangu wawili hao walipodaiwa kufumaniwa na mwanaume mwingine wa Chuchu.

No comments:

Post a Comment