Wednesday, October 23, 2013

WATANZANIA WATATU WAKAMATWA WAKIWA NJIANI KWENDA KUJIUNGA NA AL-SHABAAB NCHINI SOMALIA

Jeshi la Ulinzi la Kenya limewatia mbaroni Watanzania watatu ndani ya Somalia wakiwashuku kuwa walikuwa njiani kwenda kujiunga na al-Shabaab, gazeti la The Standard la Kenya liliripoti siku ya Jumapili (tarehe 20 Oktoba). Ali Ramadhan mwenye umri wa miaka 22, Musa Daudi miaka 19 na Shabaan Bakiri Waziri miaka 21, walitiwa mbaroni baada ya kuingia Somalia kutoka Kenya na sasa wanahojiwa katika kituo cha polisi cha Kiunga.

Polisi walisema kwamba washukiwa hao walitokea Dar es Salaam, wakasafiri hadi mpaka wa Tanzania na Kenya huko Lungalung, baadaye wakaenda kwa gari hadi Mombasa, Malindi na Lamu kabla ya kuingia Somallia.
Kwa mujibu wa polisi, watatu hao walikuwa wanaelekea Kismayu kwenda kujiunga na "vita vitakatifu, walivyodai vinaongozwa na [al-Shabaab]".

No comments:

Post a Comment