Wednesday, October 23, 2013

KUHUSU KUTIMULIWA KWA DOGO JANJA OSTAZ JUMA AZUNGUMZA, PIA DOGO JANJA ASEMA YAKE SOMA HAPA


Dogo Janja
Msanii wa Mdogo sana anayetamba katika Gemu ya Hip Hop Dogo Janja ametimuliwa tena katika Kundi la Watanashati alipokuwa anasimamiwa na Meneja Ostaz Juma na Musoma.

Akizungumza na MAASINDA BLOG Mkurugenzi wa Kundi hilo Otaz Juma amesema kuwa ameamua kumfukuza msanii huyo kutokana na Tabia zake za kukataa kusoma  pamoja na Matendo mengine ambayo hakutaka kuyaweka wazi.

" Nimeshindwana na tabia zake Dogo hajatulia hataki shule mara matendo machafu, zaidi nikiyasema hautaamini kiufupi naogopa yasitokee makubwa zaidi maana kwa sasa ni mtu mzima anamiaka 20 kwahiyo nimejitahidi kumkanya hakanyiki"
                                       Ostaz Juma akiwa na Dogo Janja 

Muandishi wa MAASINDA alipomuuliza Ostaz Juma kuhusu ushirikishwaji wa wazazi wa Dogo Janja kuhusu kumfukuza alisema kuwa alishawaambia na walienda Dar kumkanya lakini Msanii huyo hakutaka kusikia.

"Wazazi wake niliwambia na walikuja dar wakamkanya juu ya tabia zake lakini ndio hivo anazidi sasa sijui nibangi anazo vuta ndio zinamharibu"

Tulipo jaribu kumtafuta Dogo Janja kupitia simu yake ya Mkononi hakupatika lakini kupitia Blog ya DJ Choka Dogojanja alisema kuwa hajafukuzwa katika kundi hilo ila ameamua kuondoka Mwenyewe na kumtaka Ostaz Juma akitaka kuongealea swala hilo aongee na wazazi wake na sio yeye.
"Najua yatasemwa mengi kutoka kwa Ostaz Juma ila mimi ndio uwamuzi wangu, kuna watu wanasema sina utovu wa nidhamu lakini hao watakuwa wananijua sasa hivi hawajanifuatilia kutoka nyuma. Hata mtoto mdogo atakuwa mtundu ila akiwa mkubwa hunyooka na kuwa mtoto mzuri sasa nimekuwa mkubwa na kupelekwa pelekwa tena sitaki, kwa maelezo zaidi Ostaz Juma aongee na wazazi wangu asiongee na mimi"

No comments:

Post a Comment