Tuesday, October 8, 2013

MFADHILI WA COASTAL UNION 'APIGWA KISU'


               MKURUGENZI wa kampuni ya Bin Slum, wafadhili wa Coastal Union ya Tanga, Nassor Bin Slum leo amefanyiwa upasuaji mdogo wa goti katika hospitali ya Apollo mjini Hyderabad nchini India. Akizungumza na BIN ZUBEIRY kutoka Hyderabad City leo, Bin Slum ambaye hucheza soka katika timu yake ya maveterani inayofanya mazoezi Uwanja wa shule ya Msingi Muhimbili, Dar es Salaam, amesema anaendelea vizuri baada ya upasu

Nassor Bin Slum akiwa amelazwa katika hospitali ya Apollo, Hyderabad City nchini India baada ya kufanyiwa upasuaji leo 
“Namshukuru Mungu naendelea vizuri leo, ila kama unavyojua, kikubwa kilichonileta huku ni mzee wangu, ambaye amekuja kutibiwa huku, sasa nami baada ya kufanyiwa uchunguzi, nikashauriwa na madaktari, nifanyiwe upasuaji kwa sababu bado nacheza soka,”alisema Nassor. Nassor alisema kwamba aliwahi kufanyiwa upasuaji kama huo katika hospitali ya TMJ mjini Dar es Salaam miaka 15 iliyopita na hajawahi kupata maumivu makubwa tena tangu wakati huo, pamoja na kucheza soka ya ushindani kipindi chote hicho hadi miaka mitano iliyopita alipostaafu na sasa anacheza kwa kujifurahisha.
Goti la Bin Slum kushoto baada ya upasuaji

 “Mzee wangu kwa mwezi mzima nipo naye huku, kwa kweli hali yake si nzuri, na yupo chumba cha wagonjwa mahututi (ICU), kwa kweli nakabiliwa na mtihani sana, nipo katika wakati mgumu sana,”alisema, ambaye baba yake ana umri wa miaka 78.

No comments:

Post a Comment