Thursday, October 10, 2013

HIZI PICHA ZA DIAMOND NA WEMA NI NANIHIIIII!!!??? AU NDO KURUDIANA ??

Gumzo linaendelea kuhusu picha zinazosadikiwa za hivi karibuni zikimwonesha Wema Sepetu na Nasib Abdul "Diamond Platnumz" katika nyakati tofauti kwenye nchi moja huko Asia.

Picha hizi zimehusishwa na usaliti wa Diamond kwa mpenziwe wa sasa aitwaye Penny, na gazeti moja la GPL lilichapisha habari kuwa wawili hao hawapo katika 'terms nzuri' baada ya Diamond kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, Wema.

Picha zilizopachikwa hapo juu (bofya moja moja kuzikuza) zinamwonesha Diamond na staili yake mpya ya nywele ya wakati 
huu tofauti ya ya zamani. Wakati Wema akiripotiwa kuwa alikuwa China kwa ajili ya sherehe za kumbukumbu ya sikukuu yake ya kuzaliwa, Diamond aliripotiwa kipindi hicho hicho akiwa Malaysia kwa ajili ya shughuli zake za kutumbuiza na burudani. Ukiunganisha hayo yote inawezekana kabisa kupata tafsiri ya aina yake.

Lakini Diamond anasema, mpenzi wake halisi ni Penny na kuhusu picha hizi akiwa na Wema, zilipigwa tu wakati wanarekodi moja ya scenes za video ya filamu yao mpya ya ya kisanii iitwayo "Temptions". Tizama picha iliyopachikwa hapo chini kutoka kwenye ukurasa wake Diamond wa Instagram...
Hebu tujifunze kubadilika, inamaana watu mkiwa hamko kimahusiano ya Mapenzi basi msizungumze ama Kushiriki kwa chochote? Futeni huo uzamani na Mbadilike, inamaana Mnapenda kuona watu wanauadui... nimuda wa kufanya kazi ili Kulipa sifa na heshima Taifa la Tanzania na si kuekeana chuki zisizo nanfaida..

I REAL LOVE MY PENNY, SIJARUDIANA NA WEMA.  

No comments:

Post a Comment