Thursday, October 31, 2013

LULU AMTUKANA MWANDISHI KWENYE MSIBA.... KISA NI AMEANDIKA HABARI YA AIBU ALIYOIFANYA LULU UGENINI SOMA HAPA


  Elizabeth Michael ‘Lulu’.


MSANII nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amejikuta akiporomosha mitusi mizito ya nguoni kwenye msiba wa baba wa Miss Tanzania 2006/07, Wema Isaac Sepetu, mzee Isaac Abraham Sepetu hali iliyowafanya baadhi ya waombolezaji kumkodolea macho ya mshangao.Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.

KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel, Dar.

TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Katika tukio hilo la awali, Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa wa harambee ya kuchangia kansa ya matiti kwa akina mama iliyofanyika kwenye hoteli hiyo.
Wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya wachangiaji wote, Lulu alionekana akirudia kuchukua msosi kwa zaidi ya mara tatu (alikula sahani tatu).

TURUDI MSIBANI
Baadhi ya watu waliokuwa msibani hapo walimshangaa Lulu kwa kuporomosha matusi hayo ya nguoni wakati akijua kuwa yeye ni kioo cha jamii na baadhi ya maneno machafu aliyoyatamka hadharani hayaandikiki gazetini.

MSIKILIZE LULU
“Siwapendi nyinyi waandishi hasa wewe (akamtaja jina). ‘I don’t want your f**** story dude, go to hell with you’re f**** shit,” alisikika Lulu akitamka matusi hayo. (hatuwezi kuyatafsiri kwa sababu za kimaadili).

WAOMBOLEZAJI SASA
Mamia ya waombolezaji waliokuwepo eneo la msiba huo walionesha kushangazwa na kitendo cha binti huyo aliyejipatia umaarufu kutokana na kuigiza kwake.
Baadhi yao walidai hali hiyo haikuwa ya kawaida na huenda alikuwa ‘amepata kiburudisho’ (alikunywa pombe).
“Sasa binti si uende ndani ukakae? Hapa ni msibani halafu wewe unasema maneno kama hayo, huoni kama unasumbua akili za wenzako?” mzee mmoja alisikika akisema wakati Lulu anaondoka.
 

“Unajua hawa mastaa wa Bongo mimi nimeshawajua kwani nawafuatilia sana, wakiandikwa kwa mazuri meno thelathini na mbili nje, wakiandikwa kwa mabaya timbwili kama hili.
“Hiyo habari anayoilalamikia mimi niliiona kwenye gazeti tena ilikuwa na picha sasa alichokereka ni nini, si kweli au?” alisikika mwombolezaji mwingine.
Mwombolezaji mwingine alisema Lulu anaweza kuwa na hoja lakini inakufa kwa vile kama habari ilimkera alipaswa kumtafuta paparazi huyo kwa wakati wake au afike Ofisi za Global badala ya kujianika hadharani huku akidai siku hizi amebadilika.

KWA NINI ALIKEREKA?
Habari zilizopatikana baadaye zilisema kuwa, Lulu alihamaki kumwona mwandishi huyo aliyeandika habari zake hizo za kula sahani tatu, kwani tangu kutoka kwa stori hiyo amekuwa akitaniwa na mastaa wenzake wakimwambia ‘yeye ni mbaya sana kwenye mechi za ugenini’.
Tafsiri hiyo ni kwamba, Lulu amekuwa akila kupitia kiasi kwenye ‘minuso’ (minuso ni vyakula vya bure kwenye shughuli).

AJITENGA NA
BONGO MOVIE
Wakati huohuo, Imelda Mtema anaripoti kuwa, baada ya kufika ndani ya nyumba ya akina Wema, Lulu alionekana kutotaka kujihusisha na baadhi ya wasanii wenzake wa Klabu ya Bongo Movie Unity ambapo alijitenga.
Lulu alijitenga kwa kukaa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Wasanii wa Bongo Movie waliokuwepo ambao hawakupata nafasi ya kupiga stori na Lulu kama zamani ni Jacqueline Wolper, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Jennifer Kyaka ‘Odama’,  Rachel Haule, Kajala Masanja na Eshe Buheti.
 

Baadhi ya waombolezaji waliokuwemo walinong’ona kuhusu kitendo cha staa huyo kujitenga wakidai kweli sasa amekua.
 

 “Mh! Lulu sasa amekua jamani, naona hataki kabisa ushoga na watu, alipofika akasalimia na kwenda kukaa na wazazi wake, ni maajabu,” alisikika akisema mmoja wa waombolezaji ambaye jina lake halikufahamika.
 

Mwombolezaji mwingine alisikika akisema kuwa mabadiliko yote yanayoonekana kwa Lulu kwa sasa ni kazi ya mama Kanumba.

TUJIKUMBUSHE
Mzee Isaac Sepetu alifariki dunia Oktoba 28, 2013 katika Hospitali ya TMJ, Dar alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya kisukari.

MAZISHI YA MZEE SEPETU
Mwili wa marehemu ulitarajiwa kuzikwa jana saa kumi jioni Mjini Zanzibar baada ya kusafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam alikofia.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.

Imeandikwa na Jelard Lucas na Brighton Masalu na Imelda Mtema.

 

Source: GPL

No comments:

Post a Comment