Monday, October 7, 2013

CHONDECHONDE,UNATUMIA WASSAP (WHATSAPP)??? HII KITU NI HATARI SANA,UKIGUSA TU UNAJIMALIZA


Watumiaji wa WhatsApp mnapaswa kuwa makini na aina mpya ya utapeli unaokuja kwenye barua pepe (email) ukionesha kuwa umetoka WhatsApp na una ujumbe wa sauti (voice mail) unaopaswa kuusikiliza kwa kubofya kifute cha "Play".

Ukweli ni kuwa hiyo ni kanyaboya ambayo ukibofya itafungua link inayokutaka ku-install software nyingine ili uweze kusikiliza ujumbe huo.

Ikiwa utahadaika na kufanya hivyo, utakuwa umefungulia upenyo wa kuingiza virusi na malware kwenye kifaa chako cha kompyuta unachotumia kama vile simu, tablet, laptop na dektop.

Ili kuepukana na hatari hiyo, usibofye link hiyo kama ambavyo usingebofya link yoyote ya spam kutizama kilichomo.

No comments:

Post a Comment