Monday, June 17, 2013

WATOTO WA BABATI WAITAKA SERIKALI KUWAPATIA HAKI ZAO ZA KIMSINGI, PIA WAIMWAGIA SIFA SHIRIKA LA WORLD VISSION KWA KUSIMAMIA HAKI ZAO NA KUYATAKA MASHIRIKA MENGINE KUIGA MFANO HUO

Na Elisante William
Watoto Kutoka katika kijiji cha Gorowa Wilayani Babati Mkoani Manyara wakicheza Ngoma wakati wa Sherehe za Kumbukumbu ya Mtoto wa Afrika iliyofanyika Wilayani Mwada ambapo watoto wa Mkoa Mzima wa Manyara walisherehekea Siku yao katika wilaya hiyo, wakidhaminiwa na Shirika la Kusaidia watoto na jamii kwa Ujumla. Katika Kumbukumbu hizo watoto waliitaka Serikali kuwasaidia kupata haki zao za Msingi.
 Watoto Mkoani Manyara wa Wilayani Babati na Mwada wameitaka Serikali kusimamia Watoto wote kupata haki zao za Msingi, kama Kusomeshwa bila ubaguzi, pamoja na kulindwa kutokana na watu wasiokuwa na huruma wanao Wabaka, Kuwarubuni pamoja na kuwaajiri badala ya kuwasomesha.

Akizungumza na MAASINDA, Mtoto Paskalina Bwai alisema kuwa, ni vitendo vingi ambavyo vinawatokea watoto katika jamii yao kwa sanasana ni kwa watoto wakike ambao Mara nyingi ndio wanabakwa na kurubuniwa, na hivyo akaitaka Serikali kuingilia kati ili Watoto wapatiwe haki zao za Msingi.

Paskalina alisema kuwa anatoa Shukrani zake kwa Shirika la WORLD VISSION kwa kuonyesha ukaribu zaidi kwa watoto kwa kuwasaidia kupata haki zao za Msingi na uyataka Mashirika Mengine Kuiga Mfano wa WORLD VISSION.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Babati Bw, Khalid Mandia alisema kuwa Serikali inajitahidi na itaendelea kujitahidi kuhakikisha kuwa Watoto wanapatiwa haki zao za Kimsingi na kuwachukulia Hatua kali za Kisheria Watu wanaowaharibu Watoto.

Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hakusita kusema yake ya Moyoni kwa kulishukuru Shirika la WORLD VISSION kwa kuonyesha Upendo kwa Watoto na kuifanya Sherehe hiyo kuwa na Mvuto na kufurahiwa na Watoto waliohudhuria.
Mkuu wa wilaya ya Babati Khalid Mandia  akihutubia Watoto waliohudhuria katika Maadhimisho ya Mtoto wa Afrika
Wadau Kutoka katika Shirika la WORLD VISSION wakifwatilia kwa Makini Mchezo ya watoto katika Sherehe hizo

Kauli Mbiu katika Maadhimisho hayo ilikuwa ni KUONDOA MILA ZENYE KULETA  MADHARA KWA WATOTO NI JUKUMU LETU SOTE, na kauloi hiyo ilikuwa katika kila Fulana zilizovaliwa na  watoto waliohudhuria katika Sherehe hizo ambazo zilitengenezwa na Shirika la WORLD VISSION.

Kikundi cha Ngoma cha Wazazi wa watoto kikitoa Burudani Mbele ya Mkuu wa wilaya na Watoto waliohudhuria

Mwisho Kabisa WORLD VISSION ilihakikisha kuwa watoto wanakula na kushiba kabla ya Kuondoka na baadaye iliwasafirisha Mpaka Nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment