Thursday, June 6, 2013

VYAMA VYA UPINZANI VYANUIA KUUNGANA 2015


Vyama vya siasa vyenye idadi ndogo ya wanachama nchini vimekubali hatua ya kuungana na kuwa Muungano wa vyama (Alliance) kwa lengo la kupata nguvu ya uwakilishi wa kuingia katika Bunge Jipya la Shirikisho baada ya rasimu mpya kupitishwa kwa ajili ya uchaguzi ujao.

Hatua hiyo imekuja baada ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya kutangaza rasimu iliyotoa mwelekeo wa kupatikana kwa Katiba Mpya ya Tanzania.

Akizungumza jana na gazeti la Mwananchi, Katibu Mkuu wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Samweli Ruhuza amesema hali hiyo inaweza kuleta changamoto kubwa hivyo muda sahihi wa vyama vichanga kuzungumzia hili ni sasa.

Katibu mkuu wa chama cha Kijamii (CCK), Renatus Muhabi anaunga mkono hatua ya kuunganisha vyama hivyo kwa lengo la kuwakilisha mawazo yao kwa maslahi ya taifa.

No comments:

Post a Comment