Thursday, June 6, 2013

Kilimanjaro Music Awards 2013 Kuonyeshwa Live Mtandaoni








Usiku wa tuzo za Muziki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya Jumamosi, Juni 8. Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa

Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu

watumiaji wa mtandao wa Internet wataweza kuangalia toka mwanzo tukio la Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na watu

wengine mashuhuri wakiwasili ukumbini.





Pia tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa moja

kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. Watumiaji wa simu za

Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application

ya LIVESTREAM itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia http://new.livestream.com/KTMA2013 na katika Blogs mbalimbali.





Pia picha za matukio yatakayokuwa yakijiri ukumbi zitapatikana kupitia

ukurasa wa Instagram wa Kilimanjaro Premium Lager ambao ni www.instagram.com/kili_lager wakati ule wa Twitter www.twitter.com/kili_lager utakuwa ukitoa habari zinazoendelea na washindi wa tuzo na itapatikana pia katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager.

No comments:

Post a Comment