Baba Langa leo nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar |
Baba mzazi
we Langa, Mangisemi Kileo ameeleza chanzo cha kifo cha mwanaye ambaye kimetokea Jana katika Hospitali ya Muhimbili.
Langa
amefariki dunia leo katika hospitali ya Muhimbili baada ya kulazwa usiku wa
kuamkia jana.
Imeelezwa
Langa alifikishwa hospitalini hapo akiwa amezidiwa na moja kwa moja akafikishwa
katika chumba cha watu mahututi.
Salehjembe
ilifika nyumbani kwao marehemu eneo la Mikocheni Regency dakika chache baada ya
taarifa za msiba na kuzungumza na baba yake mzazi, Mengiseni Kileo.
Kileo
alisema Langa alizidiwa ghafla juzi, wakamkibiza katika Hospitali ya Kairuki.
“Pale
walituambia kwamba anasumbuliwa maralia kali pamoja na ugonjwa wa uti wa
mgongo.
“Hivyo
tukalazimika kumkimbiza Muhimbili ambako alifikishwa katika chumba cha watu
matuhuti (ICU), leo ndiyo mauti yamemkuta,” alisema.
Kuhusiana na
mazishi, Kileo alisema wanalazimika kumsubiri mkewe, Venus ambaye anatarajia
kutua nchini kesho au keshokutwa.
“Mama yake
yuko Marekani, hivyo tutamsubiri lakini tumeshazungumza naye.
“Sisi tutakaa
leo kujadili suala hilo na wanafamilia na baadaye tutajua kila kitu,” alisema
Kileo akionyesha utulivu.
Langa
alikuwa akitamba na nyimbo yake mpya ya Rafiki wa Kweli iliyotengenezwa katika
studio za Bongo Record chini ya P Funk.
Msanii
huyo alianza kutamba baada ya kushinda usakaji vipaji chini ya Coca Cola na
kuunda kundi la Wakilisha akiwa na Shaa au Sarah na Witness wakianza na wimbo
wao wa kwanza ‘Hoi’.
No comments:
Post a Comment