Monday, May 6, 2013

TRA YAWAPA SOMO WAFANYA BIHASHARA JUU YA ULIPAJI WA KODI KIDIGITALI

 Wafanya Biashara Jijini Dar es Salaam wamepewa Somo juu ya namna ya ulipaji kodi kwa njia ya Digital zaidi inayofahamika kama (EFD) jambo ambalo litasaidia kukusanya Kodi nyingi zaidi kupitia Mfumo huo.


Akizungumza wakati wa Semina hiyo iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Bluer Pearl jijini Dar es Salaam, Muelimishaji katika Semina hiyo Bw Hamis Lupenja kutoka (TRA) amesema kuwa ili kufanikisha tukio hilo kila Mfanya Bihashara atapatiwa Mashine maalumu ambayo itamsaidia kukusanya mauzo yote na kuweza kulipa Kodi kwa Uaminifu ambapo Mashine hiyo itakuwa inatoa Risiti yenyewe.

Amesema kuwa Mfanya bihashara anatakiwa kutoa Risiti kwa Mteja ili awe na uhakika na uhalali wa bidhaa zilizonunuliwa.


Ameongeza kuwa kwa Mfanya Bihashara kutoa Risiti itamwezesha kuwa na uhakika  kuwa  kodi waliolipa kwenye Bidhaa imefika Serikalini.

Aidha Mamlaka ya Mapato Tanzania imewataka wafanya Bihashara wote kwa ujumla kwa kila mmojammoja  kumuelimisha Mfanya bihashara mwenzake juu ya Umuhimu wa matumizi wa Mashine za kodi pamoja na Kuhakikisha kuwa kila Mfanya bihashara anasajiliwa ili na kupata Mashine ya kodi kulingana  na aina ya Bihashara yake.

Mfumo huo unatarajiwa kuanza kutumika kuanzia 15 MAY 2013 ambapo TRA inategemea kusajili wafanyabihashara.

No comments:

Post a Comment