Tuesday, May 7, 2013

TRA YAENDELEA NA SEMINA ZAKE JUU YA ULIPAJI KODI KIDIGITALI,, LEO IMEKUTANA NA WAHASIBU NA WASHAURI WA KODI DSM

Afisa Elimu Mwandamizi  wa (TRA) Bi,  Alvera Ndabagoye  Akizungumza katika Warsha iliyowakutanisha Wahasibu, Wakaguzi, pamoja na Washauri wa Kodi Jijini Dar es Salaam.
 Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)  leo imetoa Semina kwa mara Nyingine  kwa  Wahasibu, Wakaguzi na Washauri wa Kodi  Jijini Dar es Salaam ambapo Warsha hiyo imefanyika katika  Hoteli ya Protea  jijini Humo.

Akizungumza katika Warsha hiyo Afisa Elimu Mwandamizi  wa (TRA) Bi,  Alvera Ndabagoye amesema kuwa lengo la kukutana na Wadau hao ni kuwaelimisha juu ya Umuhimu wa Mashine hizo ili waelewe na waweze kwenda kuwaelimisha Wafanyabihashara wakati wanawashauri kulipa Kodi.

Bi Ndabagoye amesema kuwa, Mfumo huo unatarajia kuanza kutumika kuanzia May 5 Mwaka huu ambapo amesema kuwa wanatarajia kuanza na wafanyabihashara sio chini ya Laki Mbili.
Naibu Kamishna wa Idara ya Kodi za Ndani (TRA) Bi, Generose Bateyunga, akizungumza machachache katika Warsha hiyo ambapo amewataka wafanya bihashara kuelewa umuhimu wa kifaa hicho kwani kitamsaidia kulipa Kodi kwa Usawa bila kudanganywa wala kujidanganya Mwenyewe.

Afisa Elimu Mwandamizi Mkuu wa TRA Bw, Hamisi Lupenja akiwasilisha Mada ya umuhimu wa Kifaa hicho Kinachofahamika kwa jina la Electronic Fiscal Devices (EFD). 

Hiki ni Kipeperushi kinacho onyesha Kifaa hicho kitakavyokuwa.

No comments:

Post a Comment