Monday, May 6, 2013

HIVI UNAJUA KWAMBA MSANII WA HIP HOP KALA PINA AMEMPIGA MSANII MWENZIE CHIDI BENZ? EMBU SOMA HAPA NA UMSIKILIZE KALA PINA AKIZUNGUMZA KILICHOTOKEA NA SABABU ZA KUMPA ZA CHEMBE MWENZIE

"Ukweli ni mambo ya fedheha, mdogo wetu Chidi Benz, nnacho weza kusema mdogo wetu ni kwamba unga anaovuta sasa hivi unampeleka pabaya umeona eeh, tena mimi kama kaka yake namshauri aachane na matumizi ya madawa ya kulevya kwasababu mwisho wake utampeleka pabaya, mimi niko back stage nna show yangu nipo kazini, tupo seious watu wa hiphop, miaka mingi tulikuwa tuna nadi amani hatutaki matatizo na watu unaona bana, 
Tumeandaa show yetu nzuri, ilikua bonge ya show moja kali ya hiphop Tanzania kuwahi kutokea, show ambayo imekutanisha wasanii wakali wa hiphop ambao sasa hivi wanavuma, mi niko back stage naskia sauti ya Chidi Benz ameshika mic, muda ambao mi 
natakiwa kuwa stage naperfom , mi nikawaambia watu wangu vipi, huyu mtu mbona mnamuachia anatuharibia show? 

.Watu wakawa wanashindwa kumfanya kitu wakiangalia huyu ni mtu maarufu anajulikana, watu wakawa wanamplease kiustaarabu, Chidi eeh shuka hii show haikuhusu, sasa watu walivyokuwa wanamplease akawa anaona labda watu mafala au nini umeona eeh.

sasa mimi kitendo kimechukua kama dakika saba au nane hivi, bado yuko tu stage ameng'ang'ania, ananichelewesha mimi muda wa kuperfom, watu wanataka kuona show yangu, watu wamelipa hela zao, wameacha shughuli zao waje kumuona kalapina, ye anataka kukwaza watu wasimuone Kala pinia, huyu mtoto si adui jamani?" amesema Kala Pina na baada ya hapo ndipo akaamua kumshushia kipigo Chidi Benz 



MSIKILIZE KALAPINA HAPO CHINI...
  


No comments:

Post a Comment