Sunday, May 5, 2013

MTOTO MCHAWI AKAMATWA:: AKIRI KUFANYA MAPENZI NA MAJINI 12 KWA SIKU


 Hapa mtoto Naomi Mwenye umri kati ya miaka 12-14 akitoa vifaa vyake vya Uchawi.Picha na Lewis Mbonde
 Hapa ni sehemu yake ya kuondokea kwenda kufanya uchawi vitu vyake vikiwa vinaungua baada ya kuchomwa moto
 Hapa wanamaombi wakivichoma moto vitu vya Kichawi vya Naomi
 
Ni jambo la kusikitisha na la kweli lililotokea katika kata ya  Kihesa Mkoani Iringa, ambapo  Mtoto mmoja aliyefahamika  kwa jina la Naomi  anayelelewa na shirika lisilo la kiserikali la Compassion,Kituo cha Kihesa amestaajabisha jamii kwa kukutwa na vitu vya Kichawi nyumbani kwao pasipo mama yake kufahamu chochote.
 
Chanzo chetu cha habari kimetutonya kuwa mtoto huyo alikuwa na mambo yasiyo ya kawaida tangu muda mrefu sana, ambapo kilisema kuwa  maendeleo yake shuleni ni hafifu pia ana tabia ya kutoroka nyumbani na shuleni na kuelekea pasipojulikana.

"Wakati mwingine huwa anakutwa umbali mrefu sana akiwa amezubaa tu njiani hana uelekeo, Chanzo kinasema kuwa wakati wa maombi mototo huyo huwa kama ni mtu aliyezama sana kwenye maombi na hupenda sana kuimbisha nyimbo za kumsifu Mungu" kilisema chanzo hicho.
 
Chanzo chetu kinaendelea kusema kuwa mtoto huyu alikuwa ni kero kwa mama yake kwa tabia yake ya kutoroka nyumbani na shuleni.
 Kilisema kuwa ilikuwa ni siku ya jumamosi ambapo watoto wote wanaonufaika na huduma ya maombi katika shirika hilo inayotolewa na kanisa la Kristo Mfalme  hukutanika kwa ajili ya mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kiroho.
 Siku hiyo ilikuwa imepangwa kwa ajili ya maombi ya pamoja na vituo vingine yaliyofanyika katika kanisa la kristo mfalme Mjini Iringa mtoto huyo hakuwekwa katika orodha ya kati ya watoto waliochaguliwa katika msafara huo na mara nyingi katika matukio kama hayo ya kutoka nje ya kituo huwa ni king’ang’anizi sana hata akiachwa hukutwa katika eneo la tukio bila ya kujulikana kuwa amefikaje. 

"Siku hiyo ilikua ya kushangaza kidogo kwani walihakikisha amezuiwa na kuachwa kituoni lakini walipofika tu katika geti la Kanisa la Kristo mfalme umbali wa kilomita 7 walimkuta mtoto huyo ameshafika na ilipopigwa simu kituoni kuuliza kama yupo wakasema sio mda mchache ameonekana kule alipoulizwa amefikaje akasema amefika kwa mbinu zake ndipo jopo la wanamaombi likakusanyika na kumfanyia maombi", Ilielezwa.
Baada ya hapo  wanamaombi wakaelekea nyumbani kwa mtoto na kutoa vitu mbali mbali vinavyosadikiwa kuwa ni  vya kishirikina kama kisu,wembe,msumari, sindano ,sahani na vingine vingi.
Mtoto naomi alipoulizwa kuwa hivyo vitu anavitumiaje alisema kua huwa anatumia  kuulia watu na kuwawangia watoto wenzake kituoni hapo bila ya kusema kuwa amekwisha waua watu wangapi lakini alifanikiwa kuwapata watoto wenzake  wanne ambao alikua anafanyanao mambo ya kichawi.

Naomi alisema kuwa ilikuwa  kila siku ikifika mida ya saa tisa mchana  ni lazima apate kitoweo ambacho amekitaja kuwa ni  nyama za watu na kunywa damu za watu.

Ameongeza kuwa amekua akifanya mapenzi na majini kumi na mbili kila siku ambapo Baada ya mazungumzo na mtoto huyo likafuatia tukio la kuchoma moto vitu vyake katika ile sehemu yake ya kuondokea kwenda kufanya shughuli zake za kichawi.

Source: Pamoja

No comments:

Post a Comment