Kampuni Maarufu Nchini na Duniani ya Kusambaza Dawa leo
imezindua kampeni mpya ya Kusambaza Dawa
zake ambapo itamuwezesha Mteja au Mgonjwa kupata Uhakika wa Dawa Hizo.
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mkurugenzi wa Mradi DK William
Mwatu amesema kuwa, Kampeni hiyo itamuwezesha Mteja kuhakiki dawa kwa
kusoma namba maalum iliyopo katika Dawa
zake na kutuma katika namba maalumu kwa kutumia simu yake ya Mkononi ili waweze kuletewa ujumbe wa Uthibitisho kuwa
Dawa hiyo ni halalai.
Dk Mwatu amesema kuwa
katika Uchunguzi wao walioufanya kwa baadhi ya Watanzania na wagonjwa
mbalimbali wamebaini kuwa Watanzania
wengi hawana uhakika na Madawa wanayoyatumia kwa kuhofia kuwa madawa hayo sio
halali.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Afya Dk Seif s Rashid amesema kuwa , kutokana na Kampeni hiyo wanaamini kuwa uingizwaji haramu
wa Madawa Feki utapungua kama si kwisha kabisa na wagonjwa watafaidi Mfumo huo
Mpya wa kuhakiki Madawa.
Dk Seif ameitaka GSK kuwa na Ukaribu zaidi na Mamlaka ya
Chakula na Dawa ili waweze kushirikiana
kwa ufasaha na kuboresha Afya za
Watanzania.
Dk Mwatu amesema kuwa,
Mteja atakapo nunua dawa,
anatakiwa kuifungua kwanza kasha kusoma Namba maalum iliyopo katika Dawa
hiyo baada ya kungwangua Mithili ya Vocha na Kuituma namba hiyo katika Namba 15629 ambapo Mitandao inayotumika ni Voda,
Tigo, Zantel na Airtel.
Hii ndiyo Nembo ya Kampeni iliyozinduliwa leo na Naibu waziri wa Afya |
No comments:
Post a Comment