MH. LEMA AKIWA KIZIMBANI |
Godless Lema, alikuwa akishikiliwa na polisi mkoani humo kwa tuhuma za uchochezi wa vurugu zilizosababishwa na wanafunzi kwenye chuo cha Uhasibu mwanzoni mwa wiki iliyopita mwenzao kuuwawa huko maeneo ya njiro jijini humo.
Mbunge huyo alikamatwa siku ya Ijumaa na kuwekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa wa Arusha, Magesa Mulongo.
Baada ya kuachiwa mahakamani hapo mbunge huyo ameongozana na wafuasi wake kwa msafara wa maandamano na mapikipiki kuelekea katika Ofisi za Chama hicho.
Credits: Mafoto & Bongoclan
No comments:
Post a Comment