Monday, April 29, 2013

MAANDAMANO YAENDELEA HUKO JIJINI ARUSHA MARA BAADA YA LEMA KUACHIWA KWA DHAMANA

Umati wa wafuasi wa Chadema wakiwa nje ya Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kufuatilia kesi ya Lema
 

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema ameachiwa kwa dhamana hivi punde baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uchochezi katika mahakama ya Mkoa wa Arusha huku maandamano yakifanyika hivi sasa katika mitaa ya Jiji la Arusha, Tanzania.

Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge huo.habarimasai.com itaendelea kukuletea Taarifa zaidi baadaye.
 
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo katika eneo la Ngarenaro.

Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kuzomea.

Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.

Mwandishi wetu anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu. 

Katika hati ya mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo inasema kwamba kosa la Lema ni ' kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi

No comments:

Post a Comment