Wednesday, April 24, 2013

INAKUHUSU KAMA UNAPENDA SIASA,ANGALIA WALICHOKIFANYA CHADEMA JUZI IRINGA

umati mkubwa  wa  wananchi  waliofika  kusikiliza mkutano  wa Chadema  Leo Iringa mjini
katibu  mkuu  wa Chadema Dkt Slaa (kushoto) akiwa na mbunge wa jimbo la Ubungo Jonh Mnyika katika mkutano wa  wabunge wa chadema waliofukuzwa  bungeni leo katika  uwanja  wa Mwembetogwa mjini Iringa
Picha kwa hisani ya mjengwa blog 
 Iringa, leo.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk Wilbrod Slaa amewataka wabunge wa CHADEMA kuendeleza ukali zaidi na kutokuogopa kufukuzwa Bungeni.

Akiuhutubia umati mkubwa wa wananchi wa mkoa wa Iringa katika uwanja wa Mwembetogwa jimbo la Iringa mjini, Slaa alisema kuwa kamwe hawatarudi nyuma katika kupigania maslahi ya Taifa.

“Tulisimama Mwembe Yanga na kuwataja mafisadi 11 akiwemo Rais Jakaya Kikwete ila hadi leo hakuna kiongozi aliyesimama na kupambana na mafisadi hao.”

Alisema CCM imeendelea kuifanyanga katiba ya Taifa hili kufanya mambo ambayo wanayajua wao na kuacha kuwatumikia Watanzania na hivyo kuwataka askari polisi na wananchi wanyonge kuungana na CHADEMA katika kulipigania Taifa la Tanzania ili lisiendelee kuwa Taifa la mafisadi wachache wa CCM.

Alisema kuwa wapo ambao wanaeneza propaganda mbaya dhidi ya CHADEMA ila ukweli ni kuwa CHADEMA ipo kwa ajili ya kumkomboa mwananchi na hivyo kuwataka watanzania kuendelea kukipa nafasi CHADEMA ili kuipokea CCM Ikulu kutokana na CCM kushindwa kuwatumikia wananchi wake. 
Dk Slaa alisema kuwa pamoja na Idara ya Usalama wa Taifa kujifanya wanajua kila jambo, wengi wao hawaijui katiba ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania na ndiyo sababu wamekuwa wakifanya mambo bila kujitambua pamoja na wabunge wa CCM wanaokwenda Bungeni kwa ajili ya kuipongeza CCM badala ya kuwatetea wananchi.

Akawataka Usalama wa Taifa kulinda raslimali za Taifa kama twiga wanaosafirishwa nje ya nchi badala ya kupambana na CHADEMA.

Pia, aliwashangaa wabunge wa CCM ambao siku zote wamekuwa wakichangia bajeti na mwisho wakishauri ama kuipongeza bila kuangalia bajeti husika ipo kwa ajili ya wananchi ama kwa ajili ya serikali na kudai kuwa wabunge wa CCM wanafanya kazi ya serikali badala ya kuwatetea wananchi waliowatuma bungeni.

Amewataka Wabunge kutumia kamusi (dictionary) katika kupambanua kauli mbalimbali badala ya kutumia nguvu kusema wabunge wa CHADEMA wametukana bungeni.

Amewaagiza Wabunge wa CHADEMA kuchapisha vitabu vya mambo ya Bungeni na kuvisambaza kwa wananchi ili wajue kinachoendelea.
Picture
Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph Mbilinyi (MR SUGU) alisema Serikali ya CCM imepotezana kiasi cha kumchukia mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM) kwa kuonyesha kusimamia ukweli kwa kuipinga bajeti ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda. “...binafsi nampongeza mbunge Filikunjombe kwa kuwa si mnafiki kama wengine.”

No comments:

Post a Comment