Waziri Kigoda (kushoto) akijadiliana jambo na Prf Mhilu |
Waziri wa viwanda na biashara Dr Abdala Kigoda amezindua
bodi mpya ya shirika la viwango Tanzania (TBS)ambapo ameipa bodi hiyo miezi
sita kupitia mwenyekiti wake Prof.Cuthbert Mhilu kuhakikisha kuwa tbs inarudi
katika hali yake ya ubora kama zamani.
Akizungumza katika uznduzi wa bodi hiyo uliofanyika katika
ukumbi wa tbs hivi leo,Waziri Kigoda alisema kua karibu asilimia 90 ya bidhaa
zinazoingizwa nchini hazina ubora na kua walaji wanatumia bidhaa chache zenye
ubora hivyo amewataka wajumbe wa bodi hiyo kuhakikisha kuwa wanapambana na
tatizo hilo kwa haraka.
“Natoa miezi sita kwako mwenyekiti wa bodi hii hakikisha kua
tbs inatoa ubora unaokubalika na kurudi katika hali yake ya zamani”,amesema Kigoda.
Aidha waziri amezungumzia suala la uajiri wa wafanyakazi tbs
na kusema kuwa tbs ina wafanyakazi wachache kulingana na nchi nyingine kama
Kenya ambapo wanawafanyakazi wa tbs zaidi
ya elfu moja wakati Tanzania ina wafanyakazi kati ya mia nne na mia tano tu
jambo ambalo linachangia kuzorota kwa shirika hilo.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi hiyo Prof.Cuthbert Mhilu amempongeza waziri kwa kuvunja bodi
iliotangulia kutokana na kutoridhishwa na ufanisi pamoja na utendaji mbovu katika shirika hilo na kuahidi kua
katika menejimenti yake atahakikisha kua kutakuwepo na mabadiliko katika
shirika hilo na kuwa watazingatia nia ya wizara katika kuzindoa bodi mpya ndani
ya kipindi hicho cha miezi sita.
No comments:
Post a Comment