Tuesday, March 26, 2013

WATANZANIA WATAKIWA KUFURIKA SIKU YA TAMASHA LA PASAKA LITAKALO FANYIKA JUMAPILI IKLI WAPOKEE BARAKA NA UPAKO

Kati kati ni Muandaaji wa Tamasha la Pasaka kutoka Msama Promotion Bw, Alex Msama na kushoto ni Msanii wa Nyimbo za Injili Solomon Mukubwa pamoja na Msanii kutoka Nchini Kongo Bw, FDaraja wakiwa katika Ofisi ya Msama Promotion huku Solomon Mukubwa akiwaelkeza waandiushi wa habari maandalizi yake katika Tamasha la Pasaka litakalo fanyika siku ya Jumapili katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Waimbaji wa Nyimbo za Injili katika amasha la Pasaka linalo andaliwa na Msama  Promotion, wamezidi kuingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya Kutumbuiza kwenye Tamasha hilo litakalofanyika siku ya Jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Miongoni mwa Wasanii walioingia jijini Dar kwa ajili ya Tamasha hilo ni pamoja na Solomon Mukubwa kutoka Nchini Kenya, pamoja na Msanii Faraja Kutoka Nchini Kongo ambapo wameahidi kushusha Upako siku ya Tamasha hilo na hivyo wamewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi kwenye Tamasha hilo.
Solomon Mukubwa amesema kuwa, ana ahidi watu kuona Uwepo wa Mungu siku hiyo kwani  anaamini kabisa kuwa Mungu amewapa Watanzania Amani kwahivyo kwa kupitia Wimbo wake wa Mfalme wa Amani Kila mtanzania atakayekuwepo siku hiyo ataondoka na Amani.

 Aidha Mkurugenzi wa Msama Promotions ambao ni waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa Msanii Sipho Mwakaba kutoka Afrika ya Kusini anatarajiwa kuingia jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa na kuongeza kuwa siku ya Tamasha utafanyika uzinduzi wa albam ya kundi la Gloria Celebrations ‘Kwetu Pazuri’ itakayojulikana kama ‘Kuweni Macho’ ambayo itauzwa siku hiyo.


Tamasha hilo ambalo litafanyika pia katika mikoa ya Mbeya Aprili Mosi, Iringa Aprili 3, Aprili 6 mkoani Dodoma na Mwanza Aprili 7.

Viingilio katika tamasha hilo kwa VIP ni shilingi 50,000, Viti maalum shilingi 10,000, Viti vya kawaida 5000 na watoto shilingi 2000.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

No comments:

Post a Comment