Thursday, March 7, 2013

WANAWAKE WATAKIWA KUPENDANA NA KUSHIRIKIANA

Mbunge Viti Maalum Manispaa ya Ilala kwa tiketi ya CCM B, Aisha Sururu akiwa na Baadhi ya Viongozi wanawake wa (UWT) Tawi la Mtambani kata ya  Tabata katika kikao cha wanachama wanawake wa Umoja wao kilichofanyika leo katika kata hiyo ambapo Bi Aisha Sururu amewataka wanawake wao kuimarisha Upendo katika Vikundi vyao.
 Wanawake wametakiwa kupendana na Kushikamana kwa kushirikiana kwa pamoja ili waweze kujikwamua kimaisha.

Bi Aisha Sururu Mwanaharakati na Diwani katika Manispaa ya Ilala ametoa rai hiyo leo katika mkutano huo akiwa kama Mgeni wa heshima kwenye Mkutano huo.

Bia Aisha amezindua kikundi cha Vikoba kwa wanawake hao na kuwataka kuanzisha miradi tofautitofauti kwa kushirikiana na kuahidi kusaidia miradi hiyo.
Baada ya Kumaliza yake Bi Aisha aliondoka kwa kusindikizwa na wanawake hao wakiwa na furaha nyingi

No comments:

Post a Comment