Miwa ya ndani ya Kiwanda cha Sukari Mtibwa
Usoni mwa Kiwanda cha Sukari Mtibwa
Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari Mtibwa.
Na Bryceson Mathias, Mkindo Mvomero
Wakulima
Wadogo wa Miwa ya nje Kata ya Mtibwa, Wilaya ya Mvomero, mkoani
Morogoro, wamesusia Kilimo hicho na kugeuzia nguvu zao kwenye mazao
mengine kwa madai kinawapa Umaskini na hivyo kushindwa kusomesha
wanafunzi na kujikimu.
Kauli hiyo pia
ilithibitishwa jana na Mkuu wa Chuo cha Kilimo cha Mpunga Mkindo ambaye
pia ni Mkufunzi wa Mafunzo ya Shamba Darasa Bw. Moses Temi, kwamba
wakulima wengi wa miwa wanafurika chuoni hapo kupata ushauri.
Akithibitisha
wakulima kuachana na Kilimo hicho Temi alisema, kumekuwa na wimbi la
wakulima wa zao la Miwa wanaofurika chuoni hapo kutaka ushauri wa
Kitalaamu ili waachane na kilimo cha miwa na badala yake walime mazao
kama Mpunga, Mahindi na Alizeti wakidai, Miwa inawapa Umaskini wa
kifamilia.
“Ninashangaa
baadhi ya wakulima wazuri wa miwa ninaowafahamu na mashamba yao,
wamefika ofisini kwangu wakitaka ushauri wa kitalaam namna watakavyolima
mpunga na mazao mengine, na ninapowauliza kulikoni, wanadai miwa sasa
inawapa Umaskini”.
Mwenyekiti wa
Serikali ya Kijiji Kisala Msafiri Shija alisema, Kilimo hicho badala ya
kuwa mkombozi kwa wananchi, sasa kimekuwa ni sindano yenye dawa ya sumu
inayoua juhudi za wakulima wadogo na kuwanufaisha wenye uwezo, huku
walalahoi wakifirisiwa.
Hatua ya
Wakulima hao kufanywa maskini, ndiyo iliyomkera Diwani wa Kata ya Mtibwa
Lukas Mwakambaya (CHADEMA) Bunge lililopita, kutinga Mjengoni
kuwasilisha Kilio chao, jinsi ambavyo Uwekezaji wa Kiwanda cha Sukari
Mtibwa ambavyo umekuwa hauwasaidii chochote pamoja na nia njema ya
Serikali iliyowapora 25% ya Hisa yao (Share) kwa miaka yote ya uwkezaji
na hivyo kukosa sauti.
Hivi
majuzi, wakulima wadogo Miwa ya Nje Kiombero kama walivyo wa Mtibwa
walilumbana na kuilalamikia Serikali ya Wilaya Kilombero, Mkoa na
Serikali Kuu, wakidai Mwekezaji wa Kiwanda cha Sukari Kilombero (ILOVO),
kufanya wawe maskini kutokana na bei ya zao hilo kuwa ndogo kiasi cha
kushindwa kulipa madeni waliyokopa Taasisi za Fedha, ambapo Serikali
haiwashughulikii.
No comments:
Post a Comment