Sunday, March 10, 2013

TCRA KANDA YA MASHARIKI YATOA SEMINA YA MAJUKUMU YA MAMLAKA HIYO KATIKA WILAYA YA MAFIA

Hawa Sulemani  akijisomea moja ya vipeperushi vya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania baada ya kugawiwa katika semina ya Majukumu ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika katika Wilaya ya Mafia  kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo.

Baadhi ya Washiriki  wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka  ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika katika Wilaya ya Mafia  wakijisomea majaridi  yenye  ujumbe mbalimbali  na Kazi za Mamlaka hiyo. Baaada ya kugawiwa na Mhasibu wa TCRA BW.Patrice Lumumba.

Washiriki wa semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Mashariki iliyofanyika katika Wilaya ya Mafia wakishiriki katika zoezi la kutambua simu bandia.wakati walipokuwa wakionzwa na Afisa Utumishi Mkuu Esuvatie Masinga (hayupo pichani)

Mhandisi wa Masafa wa Mamlaka ya Mawssiliano Kanda ya Mashariki Stella Bunyenza akitoa mada ya Ukuaji wa Teknolojia  wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawsiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki iliyofanyika katika Wilaya ya Mafia.

Mhasibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Kanda ya Mashariki Patrice Lumumba akitoa maada ya Mfumo wa Anuani za Makazi na Posti Kodi wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika Wilayani Mafia.


Mkuu wa Wilaya ya Mfia Sauda Mtondoo akimkabidhi  Prudence Nyombi zawadi ya King’amuzi cha Star timu baada ya kujishindia kutokana na kujibu swali aliloulizwa juu ya matumizi ya Mawasiliano, wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawasiliano Kanda ya Mashariki iliyofanyika Wilayani Mafia.katikati ni Mkurugenzi wa Watumiaji na Watoa Huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema akishuhudia.

Mkurugenzi wa Watumiaji na Watoa Huduma za Mawasiliano Dk. Raymond Mfungahema akimkabidhi zawadi ya simu aina ya Nokia Mkuu wa Wilaya ya Mafia Bi,Sauda Mtondoo wakati wa Semina ya Majukumu ya Mamlaka ya Mawsiliano Tanzania (TCRA)Kanda ya Mashariki iliyofanyika katika Wilaya ya Mafia.

No comments:

Post a Comment