Tuesday, March 5, 2013

VIDEO INAYOMUONESHA MSANII WA FILAMU BONGO ( SHAMSA FORD) AKIJIFUNGUA YAVUJA NA KUSAMBAA...

VIDEO inayomuonesha msanii wa filamu Bongo, Shamsa Ford 
akijifungua imezua kizaazaa baada ya mtu asiyejulikana
 kuichukua bila ridhaa ya mhusika na kuisambaza kwa watu mbalimbali. 
 
Akizungumzia  suala hilo  hivi karibuni, rafiki wa karibu
 wa Shamsa alisema kuwa, video hiyo msanii huyo
 alirekodiwa kwa ajili ya kumbukumbu zake lakini
 ameshangaa kusikia kuna baadhi ya watu wanayo. 
“Yaani video hiyo imezua kizaazaa, Shamsa anahaha
 kumjua aliyeisambaza lakini pia anahakikisha 
haiwafikiii watu wengine na vyombo vya habari
 kwani inamuonesha hatua kwa hatua akijifungua,” 
kilisema chanzo hicho 
Baada ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta
 Shamsa ambaye alisema:“Kiukweli nimeumia sana, 
hiyo video ni kwa ajili ya kumbumbuku zangu, 
kwa nini mtu aichukue na kuisambaza bila
 ridhaa yangu? Imeniletea matatizo makubwa.”

No comments:

Post a Comment