Wednesday, March 20, 2013

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LIMEZINDUA VIPINDI VYA REDIO KATIKA KANDA YA ZIWA KWA AJILI YA KUELIMISHA JAMII HIYO JUU YA WATU WENYE ULEMAVU WA NGOZI (ALBINISIM)

Balozi wa Canada nchini Tanzania Bw, Alexandre Leveque Kushoto akitizama ramani maalum wakati alipofika katika Shirika lisilo la Kiserikali la Under The Same Sun la kutetea haki za watu wenye Albinisim ambapo alifika katika Shirika hilo kwa ajili ya Kuzindua Rasmi Mradi wa Redio wa Shirika hilo utakaokuwa unatoa elimu kwa jamii juu ya kutambulika kwa watu wenye Albinisim. Kulia ni Meneja Mipango wa UTSS Bw, Gamariel Mboya na anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa UTSS, Bi Vicky Ntetema.
 
Katika Kuhakikisha kuwa Unyanyanyasaji kwa walemavu wa Ngozi unakoma kabisa Ncxhini, Shirika la Under  the same Sun  UTSS limezindua Mradi wa Radio katika kanda ya ziwa ambapo Imani za Kishirikina dhidi ya Walemavu wa Ngozi (Albinisim) umeshamiri.
Akizungumza Mbele ya Waandishi wa habari, Meneja  wa Mradi huo Bi, Rachel Moyo, amesema kuwa,  Mradi huo utakuwa katika Redio zilizopo Kanda ya Ziwa na Redio hizo zitakuwa na Vipindi vya kuelimisha jamii vitakavyojulikana kwa jina la Tambua albinisim, na vitarushwa kwa Mtindo wa Makala mchanganyiko, Majadiliano ya Moja kwa Moja ikiwa ni pamoja na Mchango wa simu kutoka kwa Wasikilizaji pamoja na Mchezo wa Kuigiza.
Bi, Rachel amesema kuwa Mradi huo umedhamini wa na  kwa ushirikiano wa Serikali ya Canada kupitia Ubalozi wa Canada ambapo  walichangia kiasi cha Dola 20,000 za kimarekani sawa na milioni 30 za Kitanzania.
Balozi wa Canada nchini Tanzania Bw, Alexandre Leveque akifungua kinywaji kama ishara wa Uzinduzi Rasmi wa Vipindi hivyo(Mradi huo) Wengine ni Mkurugenzi wa UTSS Bi Vicky Ntetema pamoja na Viongozi wa Shirika hilo.

No comments:

Post a Comment