Thursday, March 21, 2013

CHADEMA WAITAKA SERIKALI KUWAPATIA MSAADA WAATHIRIKA WA KIMBUNGA KATA YA KAJOHE


KATIBU Mkuu wa Jimbo la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Jumaa Mwipopo, ameitaka  Serikali kuhakikisha kuwa inawapatia msaada waathirika wa kimbunga kilichotokea Kata ya Majohe wilayani Ilala, Mach tatu mwaka huu.

Katibu alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza ba wandishi wa habari kuhusu kitendo cha Halmashauri hiyo kukaa kimya hadi leo kwa kutopeleka msaada tangu kutokea kwa tukio hilo.

Mwipopo alisema kimbuka hicho cha upepo kilichotokana na mvua kubwa kilisababisha kubomoka nyumba zipatazo 176 katika mitaa ya Nyeburu, Zavala na Kigenzi katika kata hiyo.

Alisema wanatoa siku saba kuiomba Halmashauri hiyo na serikali kuwa  inawapatia misaada ya chakula ikiwa ni pamoja na kuwajengaewa makazi yao, hawana uwezo wa kujenga, ili warudi katika maisha yao ya kawaida kama wengine.

Mwipopo alisema endapo itashindikana basi wataitisha mkutano ili wa waeleze wakazi hao wa Nyeburu na Zavala kuwa serikali yao imeshindwa kuwasaidia ama huenda ikawa inawachukulia kuwa wao si sehemu ya Watanzania hivyo hawana haki ya kupata msaada.

“Inasikitisha kutokana na kubaguliwa na kutowapa msaada wowote yakaribia mwezi sasa, wakati waathirika wa mabomu Mbagala Waziri Mkuu alichangasha fedha kwa kuwaita wakurugenzi wa Halmashauri na Mameya na kuwaamuru wachangie milioni 20 kila halmashauri kwa ajili ya waathirika wa Mbagala na yetu ilitoa fedha hizo iweje kwetu ishindikane”alisema Mwipopo.

Mwipopo alifafanua kuwa mwaka 2012/13, zilitengwa fedha katika ofisi ya Meya kwa ajili ya misaada kwa jamii, zilitengwa jumla ya milioni 21.8 ambako kazi yake ni kwa ajili ya majanga kama haya yanapotokea.

Aidha, taarifa yao hiyo imesambazwa kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu wa Chedema Taifa, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Meya wa Manispaa ya Ilala.

Ni hivi karibuni Mkuu wa Mkoa alisikika kuna matatizo mengine yakondani ya uwezo wao wanachi, kwani kama serikali ikiyaendekeza itajikuta mwaka mzima ifanyakazi hiyo.

No comments:

Post a Comment