Friday, March 15, 2013

SHINDANO LA REDD’S MISS TANZANIA 2013 LAZINDULIWA

Baadhi ya
Warembo walioshirikishi Shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 wakicheza muziki
wa aina ya Kwaito wakjati wa tafrija maalum ya uzinduzi wa Mashindano ya Miss
Tanzania 2013 Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam Machi 14, 2013. Kulia ni
Redd’s Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred.
 Redd’s
Miss Tanzania 2012, Brigit Alfred (katikati) akigonganisha glass na
Mkurugeni wa Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) ambao ni Wadhamini
wakuu wa Shindano la Miss Tanzania,Kushilla Thomas (klia) pamoja na
Mkurugenzi wa Lino International Agency waandaaji wa Miss Tanzania,Anko
Hashim Lundenga ikiwa ni ishara ya uzinduzi rasmi wa mbio za kumsaka
Mrembo wa Redd’s Miss Tanzania 2013 wakati wa tafrija mchaparo a.k.a
mkia wa jogoo (cocktail party),iliyofayika usiku huu kwenye Ukumbi wa
Maqee,uliopo Serena Hoteli,jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Lino International Agency ya Jijini Dar es Salaam, ambao ndio
waandaji wa Shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga akitoa hotuba ya
ufunguzi, wa Shindano la kumsaka Malkia wa Tanzania 2013.
Hii ndio ilikuwa tatu bora ya Miss Tanzania 2012,Mshindi wa Taji la Redds Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred (katikati) akiwapamoja na washindi wenzake, Eugene Fabian aliyetwaa nafasi ya pili (kulia) na Mshindiwa Tatu, Edda Sylvester
 Mlezi wa
Kamati ya Miss Tanzania, Mzee Ole Naiko (kulia) akizungumza na wanakamati ya
Miss Tanzania na Miss Tanzania 2012.
 Redds Miss
Tanzania 2012, Brigit Alfred akitoa hotuba ya ufunguzi, wa Shindano la kumsaka
Malkia wa Tanzania 2013.
 Banana Zoro na kundi zima la B Band lilitoa burudani
 Kazi ni kwako
 Mambo ya burudani yalikuwa si mchezo, Uncle Lundenga na my wife wake wakisakata rumba toka B Band.
 Wadau wa Miss Tanzania walikuwepo kuunga mkono shindano hilo.
Mkurugenzi wa Excutive Solutions,Aggrey Maliale akibadilishana mawazo na Meneja Masoko wa TBL,Mamungai.
 Mdau na Mwandaaji wa Miss Musoma, Godson Mukama (kulia) akiteta jambo na Fimbo Butala wa TBL.
 Warembo hii ilikuwa shughuli yao.

No comments:

Post a Comment