Friday, March 15, 2013

SAKATA LA KUKAMATWA LWEKATARE, CHADEMA WATAKA POLISI KUFANYA UCHUNGUZI

Lwakatare

 
Dkt Slaa
Siku moja baada ya kukamatwa na kushikiliwa na vyombo vya usalama kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) WILFRED LWAKATARE kwa tuhuma za kuhusika na mashambulizi ya watu mbalimbali chama hicho kimelitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa suala hilo pasipo kuingiliwa na wanasiasa.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ambao pia ulihudhuriwa na baadhi ya wabunge wa CHADEMA, Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. WILLBROAD SLAA amesema anashangazwa na hatua ya jeshi la polisi kumkamata kiongozi huyo wa CHADEMA kwa kuona picha kwenye mtandao wakati zipo taarifa nyingi za uchochezi zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii kuwahusu watu mbalimbali ambazo hazijachukuliwa hatua.

Amesema haamini kama kiongozi huyo wa CHADEMA anaweza kupanga mipango ya kufanya uvunjifu wa amani licha ya kuiona picha ya video iliyowekwa kwenye mtandao, ambayo amedai haina ushahidi wa kutosha.


 

No comments:

Post a Comment