Monday, March 11, 2013

JESHI LA POLISI LAWASIMAMISHA KAZI MAOFISA WAKE WATANO KWA TUHUMA MBALIMBALI


WAZIRI wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi amecharuka na kuwasimamisha kazi maofisa watano wa Jeshi la Polisi nchini na kuagiza wafuguliwe kesi mara moja katika mahakama ya Jeshi.

Alisema katika tukio la kwanza lililotokea mkoani Mbeya mwaka jana maofisa watatu wamesimamishwa kazi na kutarajiwa kufunguliwa kesi kutokana na kukamatwa kwa dawa za kulevya aina ya kokein.

Alisema baada ya kukamatwa na kwenda kuifadhiwa katika boahari ya dawa ilipofika kwa mkemia mkuu iligundulika ni sukari na chumvi

"Tume iliyoundwa kuchunguza tukio hilo ilibaini kuwa kilichokamatwa na kilichopelekwa kwa mkemia mkuu ni vitu viwili tofauti " alisema Nchimbi.

Alisema katika tukio hilo aliyekuwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi- Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya Eliasi Mwita, aliyekuwa Msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa huo Mrakibu Mwandamizi wa Polisi Jacob Kiango na aliyekuwa Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia, Mrakibu Msaidizi wa Polisi Charles Kinyongo wamesimamishwa kazi.


Dk. Nchimbi ametoa mwito kwa maofisa wa jeshi la polisi kufanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria za jeshi hilo na atakayeenda kinyume atachukuliwa hatua stahiki.

Kwahisani ya Dotto Mwaibale

No comments:

Post a Comment