Friday, March 1, 2013

HII NDIO SEHEMU ALIYOKUA AMEHIFADHIWA YULE BINT ALIETEKWA KWA MIEZI MINNE

 Huyu ni mmoja wa vijana watatu waliokamatwa, walitoka Kigoma kuja Kibaha kufanya kazi ya ulinzi kwenye mashamba, huyu mkazi wa kibaha kijiji cha kidimu anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumteka msichana wa hapo kijijini kwa miezi minne kabla ya ishu kufumuka february 26 baada ya binti kupata upenyo na kutoroka.



Kwenye hayo matofali hapo ndipo alipokua analazwa binti alietekwa na kutumika kingono, mwanaume alikua akimaliza haja yake ndio anamrudisha humo ndani, vijana waliohusika ni watatu na wanashikiliwa na polisi tayari kwa kufikishwa mahakamani, stori itaendelea leo kwenye Leo Tena ya Clouds Fm.


Huyu ndio binti mwenyewe wa miaka 16 alietekwa, alipata ujauzito wa miezi miwili lakini vijana hao wakautoa kwa kutumia majani ya cha.
Akionyesha sehemu aliyokua analazwa.

Huyu binti alipotea toka novemba 2012 na alishatafutwa kila sehemu ikiwa ni pamoja na waganga kutumika, wazazi walishaomba sana kanisani na kukata tamaa wakijua binti yao ameshakufa mpaka wakaweka msiba kabisa.

No comments:

Post a Comment