Tuesday, March 26, 2013

Diwani Chadema azuia Michango, yamnyakua Balozi wa CCM


.Diwani wa Kata ya Mtibwa Luka Mwakambaya akizungumza na wananchi wa kijiji cha cha kidudwe


Bryceson Mathias, Kidudwe Mvomero.

Diwani wa Kata ya Mtibwa kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Luka Mwakambaya, katika mkutano wa hadhara uliofanywa Kidudwe wilayani Mvomero, amewazuia wananchi wake wasichange michango kwa sababu ya Njaa.

Akizungumza na wananchi waliofurika mkutanoni hapo Mwakambaya alisema, kutokana na njaa iliyoikumba Kata hiyo, wananchi wake wasichangishwe michango ya maendeleo ili  fedha chache walizonazo, watumie kununulia chakula wapate wajikimu hadi mwezi Agosti.

Hatua ya Mwakambaya ya kutoa Katizo hilo ilitokana na Ugumu wa maisha uliopo ambapo Debe la Mahindi katika Kata hiyo kwa sasa limefikia Sh. 16,000/-, hali ambayo imewasababisshia wananchi hao kuwa na wakati Mgumu.

Hata hivyo Mwakambaya alisema, kila Mtaa, Kitongoji na Vijiji vya Kata yake, viorodheshe Idadi ya Wananchi wenye uwezo wa kuchangia Maendeleo ili mwezi huo ukifika waweze kuchangisha Machangizo yenye tija mara moja.

Mwakambaya aliwanyoshea kidole na kuwaonya watendaji wasiwe Miungu Watu kwa kwa kuwatoza wananchi, Sh. 10,000/- hadi 15,000/-  kama ada ya kuwakamatia waharifu kabla ya kuwafikisha Polisi.

Katika Mkutano huo aliyekuwa Balozi wa Kitongoji cha kwa Sungura, Christopher Laurent Mkonomali (CCM), alitangaza kujiunga na Chadema ambapo alijinadi akisema “ Mimi na Ubalozi wa CCM sasa basi nimehamia Chadema”. Alisema Mkonomali.

Aidha Mkonomali alirudisha Kadi ya CCM Na. AA575657 ya Januari 8, 2008 na kukabidhiwa ya Chadema Na. CDM.250713 na Diwani wa Viti Maalum Juliana Petrol ya Machi Machi 26, 2013.

No comments:

Post a Comment