Watu ambao hawajafahamika waliwarushia bomu maofisa
usalama waliokuwa wanailinda lango la kuingilia kwenye kituo cha kuhesabia
kura katika mji wa Wajir Jumanne usiku (tarehe 5 Machi), na kumjeruhi
polisi mmoja anayefanya kazi katika idara ya ukaguzi wa ndani.
Washambuliaji hao walilenga bwalo la halmashauri ya wilaya ya Wajir
muda kama wa saa 2:00 usiku, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Wajir James
Mutungi aliiambia Sabahi. Alisema ofisa aliyejeruhiwa alikuwa miongoni
mwa maofisa waliosambaza katika eneo hilo kuimarisha usalama katika
bwalo hilo, ambapo kura za jimbo la Wajiri Mashariki zinahesabiwa hapo.
Alisema Bomu hilo lilirushwa muda mfupi baada ya Mbunge wa Wajiri Mashariki kutangazwa kuwa mshindi.
"Polisi wanachunguza shambulio hilo lakini hakuna aliyekamatwa," Mutungi alisema.
Mratibu wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka kwa jimbo la Wajir Mashariki
Andrew Njoroge alisema alikuwa akijitayarisha kutangaza matokeo ya
nafasi za urais, magavana, useneta na wawakilishi wa wanawake wakati
mlipuko huo ulipotokea.
"Ni kutosikia vizuri na sitaeleza mahali halisi ilikotokea hadi
maofisa usalama waifanye hapo kuwe salama," alisema Mratibu huyo, akiongeza
kwamba tukio hilo halikuzuia tangazo hilo.
Chanzo Mitandao
No comments:
Post a Comment