Mtoto Ombeni akiwa amelazawa katika Hospitalini ya General mjini Dodoma akipata matibabu baada ya kupata ajali ya moto Desemba 14 2012. Pichani mmiliki wa blog ya Pamojapure akimfariji mtoto Ombeni baada ya kumtembelea hospitalini alikolazwa.
*******
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Wakati
hali ya mtoto Ombeni Mbeula ambaye amelazwa katika Hospitali ya General
iliyopo mjini Dodoma ikiwa bado si nzuri baadhi ya wadau wameanza
kujitokeza kwa ajili ya kumpa msaada wa kupata matibabu.
Mtoto
Ombeni ambaye alipata ajali ya moto huko Mpwapwa alifikishwa
hospitalini hapo tarehe 14/12/2012 kwa sasa mtoto huyo ameanza kupata
matibabu baada ya habari zake kurushwa kwenye mitandao ya kijamii ambapo
kwa sasa madaktari wa hospitali ya General wameanza kumpatia matibabu
mtoto huyo baada ya kukosa huduma hiyo kwa kipindi cha miezi miwili
kutokana na wazazi wake kukosa fedha za matibabu.
Kwa
moyo wa dhati tunawashukuru wale wote waliotoa michango yao kupitia
kwenye namba ya ndugu yake ambayo ni Ekiria Paskali na namba yake ya
simu ni 0757 498336 Hawa ni baadhi ya wale walioguswa na tukio hilo na
kutoa mchango wao wa hali na mali.
Kwa
mujibu wa habari kutoka kwa mmiliki wa Blog Pamojapure michango
iliyopatikana kutoka kwa wadu ni jumla ya shilingi 421,300 ambazo
zitamsaidia mtoto huyo katika matibabu yake na wadau wameombwa
kujitokeza ili kunusuru maisha ya mtoto huyu. Kama umeguswa na matatizo
ya mtoto huyu unaweza kumchangia mtoto huyu apate matibabu tuma mchango
wako kwa kutumia namba hii 0757 498336 mwenye jina lake ni Ekiria
Paskali
No comments:
Post a Comment