KATIKA hali ya kawaida, tumezoea
kuona watalii kutoka mataifa mbalimbali duniani wakija nchini kuangalia vivutio
vya utalii vilivyopo.
Baadhi
ya vivutio hivi ni Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama, majengo ya kale, mapango
na nyumba za kihistoria. Hata hivyo, kumeibuka aina mpya ya utalii,
unaojulikana kama utalii wa ngono, ambao unashamiri kwa kasi ukihusisha zaidi
watalii wanawake wanaofuata wanaume wa Kitanzania hasa vijana.
Uchunguzi
uliofanywa na Mwananchi Jumapili, unaonyesha kuwa utalii huo unaongezeka kwa
kasi hasa katika maeneo yenye vivutio vingi vya utalii ikiwamo Arusha,
Kilimanjaro na Zanzibar.
Imebainika
kuwa katika utalii huu, wanawake hasa watu wazima walio na umri kati ya miaka
60 hadi 80 kutoka nchi mbalimbali, wamekuwa wakiingia nchini kwa lengo la
kutafuta vijana wa kiume wa kustarehe nao.
Uchunguzi
huo unaonyesha kuwa wanawake ambao hawana vigezo vya uzuri vinavyopendwa na
wanaume huko kwao, ikiwamo wembamba na urefu, husafiri kuja Tanzania kutafuta
mwanamume atakayestarehe naye kingono. Hali hiyo inawakumba zaidi wanawake
wanene, ambao kwa Ulaya hukosa wapenzi, hivyo kulazimika kusafiri kuja Afrika
Tanzania ikiwamo kutafuta mwenza wa kustarehe nao
.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hilo umebaini kuwa, utalii huu umeshamiri ambapo vijana wa Kitanzania wanaufahamu na wamekiri kuwa umewanufaisha, na
baadhi yao kuwasaidia kupata tiketi za kwenda kuishi Ulaya.
Katika Visiwa vya
Zanzibar utalii huo unafanyika zaidi katika fukwe za Nungwi, Kiwengwa, Paje,
Kendwa, Jambiani na maeneo mengine yaliyopo pembezoni mwa bahari.
Katika
fukwe hizo vijana maalumu kwa kazi hiyo, wana kauli mbiu yao inayosema:“apewe
mpaka apagawe, atoe tiketi.”
Kwa kauli mbiu hiyo vijana hao wanamaanisha kuwa, kwa kila mwanamke
watakayekutana naye, watatumia kila mbinu ili kumfurahisha hadi awasafirishe au
kwenda naye Ulaya.
Abdulla Ali Haji (Sio jina halisi) ni miongoni wa vijana
wanaojihusisha na aina hiyo ya utalii, anayeishi visiwani humo ambapo anaeleza
kuwa shughuli yake kubwa ni kuzunguka katika fukwe mbalimbali akiwinda wanawake
wa kizungu wanaotaka kustarehe.
|
No comments:
Post a Comment